Google + (Google Plus) ni mtandao mwingine wa kijamii kutoka katika kampuni ya Google (ALPHABET). Mtandao wa kijamii huu licha ya kutangazwa sana lakini bado haujateka mioyo ya wengi
Google + ina watumiaji wachache ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook na Twitter.
Google + ilianzishwa mwaka 2011 na haikupata mafanikio makubwa kivile na hii ni baada ya mtandao wa kijamii wa Facebook na Twitter kuzidi kuteka mioyo ya watu.

Wakati Google + inaanzishwa mwaka 2011, watu wengi walikuwa hawapendi ku ‘share’ mambo yao katika mitandao ya kijamii kama sasa. Na pia kumbuka kuna baadhi ya watu walishindwa ku ‘share’ mambo yale ambayo wanataka ku ‘share’ kutoka moyoni.
Hali hii ilipelekea kwa Google + kujiuliza swali moja tuu la msingi.. Je, ni vitu gani ambavyo watu wanafanya?
Hapa waligundua kuwa watu katika maisha yao ya kila siku kuna vitu na vitu ambavyo wana ‘Share’ na watu Fulani husika. Hii ina maanisha kuwa kitu ambacho una ‘Share’ wewe na rafiki zako kinaweza kikawa ni tofauti na unacho ‘share’ na wazazi wako. Pengine kama ukitaka kukiweka kitu hicho katika mtandao utashindwa kama hao wote wawili (rafiki na wazazi) wapo katika mtandoa huo.
Google + ilipogundua hilo ikaweka makundi maalumu ambayo mtu anayatengeneza mwenyewe (circles). Yaani ukiwa unatumia mtandao huo unaweza ukatengeneza kundi unalolitaka na kisha uka ‘Share’ kitu Fulani na watu hao pekee.

Japokuwa mambo mengi na maboresho mengi sana yalifanyika ili kuhakikisha Google + inaiteka sekta ya mitandao ya kijamii lakini bado juhudi hizo ziligonga mwamba kwani Facebook na Twitter zilijiimarisha zaidi.
Ukiachana na mambo hasi ambayo Google + imeyapitia bado kampuni linazidi kujiimarisha tuu. Hivi karibuni Google + imeongeza mtu katika timu yake ambae anasemekana anaweza akaleta mabadiliko makubwa kwa kuja na ubunifu wa aina yake.
Mtu huyo si mwingine bali ni Muanzilishi wa 4Chan, Bw. Chris Poole. Bado haipo wazi juu ya nini ambacho Bw. Poole anaifanyia kampuni hiyo kwa sasa. Lakini kwa uajiri huu unaonyesha Dhahiri kuwa Google bado hawana matumaini ya kuutelekeza mtadao huo wa Google +
Kumbuka Mtandao huu umetoka mbali licha ya kwamba hauna watu wengi ambao wana utumia, Facebook na Twitter kwa sasa ndio wapinzani wakuu wa mtandao huu.
Ningependa kuona mtandao wa Google + unarudi kwa kishindo na kuleta changamoto nzuri kwa mitandao mingine ya kijamii. Hili likifanyika basi hata swala zima la Mawasiliano litakuwa rahisi zaidi