Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa magemu ya muendelezo wa GTA basi utakua ulishawahi sikia fununu kuwa mchezo huo ulikua na mpango wa kutoa toleo ambalo lingekuwa linaonyesha mitaa tofauti tofauit ya jiji la Tokyo nchini Japan. Jambo hili limebadilika, tujue sababu kubwa nyuma za pazia
Nani ambae asingependa kuona kama anaweza akacheza maisha Fulani katika gemu katika mitaa ambayo anaijua fika? Nna imani kubwa kuwa wapenzi wa magemu ya GTA wangependa kucheza gemu hilo katika mitaa wanayoijua katika maisha yao ya kawaida.
Kampuni ya Rockstar Games ambayo ndio mtengenezaji na muendelezaji wa muendelezo wa gemu za GTA imekuwa na mafanikio makubwa juu ya mchezo huo. Kila toleo ambalo waliwahi kutoa lilikuwa na mafanikio zaidi kuliko toleo la nyuma yake. Kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiboresha sekta nzima ya magemu kwa kuongeza changamoto katika teknolojia ya magemu.
Kwa kujumisha muziki, muonekano, vitu vilivyomo ndani na cha msingi ni sehemu huru ambayo mchezaji wa gemu za GTA anaweza akafanya jambo lolote. Kwa kutengeneza kitu kama hichi gemu la GTA ndio limekuwa juu katika magemu.
Ni miaka mitatu imepita tangia kampuni hilo kutoa tolea lake la GTA 5 (Grand Theft Auto: V) na kwa sasa wapo katika utengenezaji wa toleo la 6 la mchezo huo ambalo litaitwa GTA 6 (Grand Theft Auto: VI)
Taarifa ambazo zimepatikana ni kwamba kampuni ya Rockstar ilikuwepo Tokyo, Japan katika harakati za kuangalia mitaa kwa lengo la kuweka mitaa hiyo katika gemu lao. Kwa kipindi hicho hata jina la gemu la Grand Theft Auto: Tokyo lilikuwa limeshaanza kusambazwa ikiwa ikimaanisha ni toleo ambalo litafuatia.
Baada ya Rockstar kupata matatizo (ugumu) kuziweka katika ramani baadhi ya barabara za Tokyo na kwa kwa kuwa jina la Grand Theft Auto limepata chimbuko lake kutoka katika tamaduni za kiamerika. Na pia Rockstar ilikuwa na bidhaa na ‘brand’ tofauti tofauti za nyumbani ambazo zilikuwa tayari katika kupandikizwa katika toleo hilo, hata swala zima la muingiliano lilikuwa ni moja kati ya sabubu ambazo zilisitisha zoezi hilo.
Mtoaji taarifa alisema kuwa Rockstar wanabadilisha jina la gemu linalofuata na kulipa jina la Grand Theft Auto: Bogota na Grand Theft Auto: Sin City. Na kwa haraka haraka ukiangalia GTA: V ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na iliachiwa mwaka 2013 na haikupata umaarufa mkubwa sana mpaka ilipoachiwa kwa vifaa vingi mwaka 2014. Ukilinganisha na muda ambao umetumika kulitengeneza toleo hilo la tano, usije ukashangaa kuwa toleo lijalo (la sita) likachukua hata mwak wa 2020 katika kutoka