Rockstar Games Inc ndio inamiliki gemu la GTA na mengine mengi, gemu hizi ni moja kati ya magemu ambayo yanafanya vizuri sana katika soko.
Soko la magemu ni wazi linazidi kukua siku hadi siku na gemu la GTA nalo linazidi kukuwa na kuboreshwa kadri kila matoleo mapya yanavyotoka na ni zamu ya toleo la GTA 6.
Kwa sasa kampuni iko ndani ya mpango mkakati wa kuachia gemu hilo katika kipingi cha muda mfupi unaokuja na kwa kuanza wataanza na kionjo (trailer) cha gemu hilo.
Kionjo (trailer) hilo linategemewa kuachiwa mwezi disemba mwaka huu, na inasemekana kwa namna moja au nyingine litakua na mshiriki mkuu wa kike.
Wamefanya hivi kusudi ikiwa na sehemu kama ya kuwaenzi wale wapenzi na wahalifu wawili ambao walikwenda kwa jina la Bonnie and Clyde.
Kingine ni kwamba Gemu hii inadhaniwa kwamba itakua inahusu mitaa mingi ya Miami (ya kufikirika) huko marekani lakini pia kumbuka hata toleo la GTA Vice City na lenyewe lilitumia mitaa ya kufikirika ya jiji hilo.
Tangu 2013 ambapo ndio gemu la GTA 5 lilipozinduliwa rasmi mpaka sasa limeweza kuuza nakala Zaidi ya milioni 185 duniani kote na kuifanya kuwa kati ya magemu ambayo yameuzika sana.
Kampuni lenyewe lina shauku ya kutaka kuwaletea wachezaji magemu kitu kipya na hii ni baada ya miaka kumi na wanaamini gemu hili litakua la aina yake.
Kaa nasi hapa TeknoKona maana tutakuletea taarifa kadha wa kadha kuhusiana na gemu hili, ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je unadhani gemu hili litaliteka soko?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.