Marcel Lazar ambaye anafahamika kwa jina lake la mtandaoni la Guccifer amehukumiwa kwenda jela nchini Marekani kwa wiki 52, baada ya kupatikana na hatia ya kudukua na kusambaza taarifa za watu wengine pasipokuwa na idhini ya kufanya hivyo.

Kwanini Mdukuzi huyu anaongelewa na vyombo vya habari?
Guccifer ameshika vichwa vya habari vya ulimwenguni sio kwa sababu ni mdukuzi mwenye utaalamu sana la! bali kwasababu alifanikiwa kuwadukua watu wengi maarufu akiwamo raisi mstaafu wa Marekani na watu wake wa karibu.
Marcel hana ujuzi mkubwa katika mambo ya kompyuta!
Kwa taarifa yako to Marcel Lazar hana ujuzi wajuu sana wa udukuzi, ila anatumia njia ya kukisia nywila ama maswali ya usalama ambayo tunayatumia kubadilisha nywila zetu. Kuna wakati mdukuzi huyu alitumia muda wa miezi sita kudukua akaunti moja tu ya barua pepe ya mtu maarufu huko romania.
Guccifer alikwisha kamatwa na kuhukumiwa miaka 7 jela huko Romania baada ya kupatikana na hatia ya kuwadukua watu maarufu, alisafirishwa kwenda Marekani ambako nako alikuwa akikabiliwa na mashitaka kama hayo.
Marcel amewadukua nani na nani?!
Kwa mujibu wa mtandao wa WIKIPEDIA baadhi ya watu ambao ni wahanga wa udukuzi wa huyu jamaa ni pamoja na Bush raisi mstaafu wa marekani, Collin Powel aliyekuwa afisa mkubwa marekani seneta wa Maekani Lisa Murkowski pamoja na Sidney Blumenthal ambaye alikuwa mshauri wa Hillary Clinton kwa maswala ya kisiasa na alipomdukua huyu ndipo alipogundua kwamba Clinton anatumia barua pepe binafsi kwa mambo ya kazi.