BBM Kwenye Samsung |
Ulimwengu wa habari za teknolojia ulipata habari kubwa ya kuandika kuhusu tarehe rasmi ambayo mesenja maarufu ya BBM (Blackberry Messenger) kutolewa rasmi kwa ajili ya kushusha (download) kwenye simu za Android na zile za Apple (iOS).
Taarifa zilianzia kupitia tweet moja kupitia akaunti ya kampuni ya simu ya T-Mobile (Uingereza). ndani ya muda mchache habari ya tarehe hii ya kutoka kwa BBM kwa ajili ya simu zingine iliandikwa kwenye mitandao mingi.
Ila habari ya uhakika hadi sasa ni kwamba tweet hiyo ilitolewa kimakosa na ishafutwa katika tweets zao. Hivyo tutegemee lolote, BBM inaweza ikaja hiyo Juni 27 au tarehe nyingine yeyote.
Habari za uhakika hadi sasa ni kwamba BBM itakapokuja itakuja kwa ajili ya simu za Android ya toleo 4 kwenda juu, wakati kwa iOS (iPhones) ni zile zenye toleo la iOS 6+. Na hadi sasa kampuni ya BlackBerry inapigania kuona simu zijazo za iOS na Android ziweze kuja na BBM ikiwa ishaingizwa (pre-installed) kabla ya kuwafikia wanunuzi.
Endelea kutembelea Teknokona..
No Comment! Be the first one.