HarmonyOS ni programu endeshi maarufu kabisa ya Huawei ambao ni magwiji kabisa katika maswala mazima ya teknolojia.
Huawei inamiliki teknolojia nyingi sana kama vile HarmonyOS na pia inatengeneza vifaa vya kielekroniki kama vile simu janja, Televisheni n.k.
Kwa sasa kumbuka Android ndio programu endeshi ambayo inatumiwa zaidi na watu huko china huku programu endeshi ya iOS ikiwa ni ya pili.
Hili litabadilika, kumbuka mwaka jana Huawei ilishawashangaza watu kwa kiasi kikubwa sana baada ya kauchia simu janja zake za Mate 60.
Hili kwa kiasi kikubwa liko wazi kwamba wakati Android na iOS wakiwa wanazidi kukimbiza katika soko la dunia nzima lakini kwa upande wa china lazima mpasuko utokee.
Kumbuka Huawei imerudi vikali katika soko la kutengeneza simu na wamerudi katika teknolojia ya 5G kabisa, hali ambayo watu wengi wa teknolojia wanasema itakua mbaya kwa Apple.
Kumbuka simu za Huawei kwa muda kidogo zilipotea katika soko, na hii ni baada ya kupatwa na vizuizi kutoka marekani hali ambayo ilifanya kampuni kuja na program endeshi yake binafsi ambayo ni HarmonyOS.
HarmonyOS inajitegemea na inaweza kutumika katika vifaa vingi ukiachana na simu janja tuu, bado vifaa kama vile Kompyuta.
Kama vifaa vingi vikiwa vinatumia programu endeshi hiyo —HarmonyOS— nchini china kuliko iOS basi kombe litakua limeenda kwa Huawei.
Kumbuka pia serikali ya china inapinga vikali matumizi ya teknolojia ya nchi za nje kama kuna uwezekano wa kupatikana humo humo katika nchi yao.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sehemu ya comment je unadhani Huawei itaipikua Apple kwa swala hili?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.