Kampuni ya Helios Towers, inayojihusisha na uwekazaji na usimamiaji wa minara ya mawasiliano ya simu barani Afrika yajiingiza rasmi kwenye soko la hisa la jijini Landani, Uingereza.

Kampuni ya Helios Towers inamiliki na kusimamia minara katika mataifa mbalimbali Afrika na hii ni pamoja na; Kongo (DRC), Ghana, Afrika Kusini na Tanzania.
Helios wamerahisisha uwekezaji wa sekta ya mawasiliano katika miundombinu ya minara ya simu kwa kuwezesha mnara mmoja kutumiwa na mitandao mbalimbali ya simu.
Kwa sasa makampuni ya huduma za simu yanakuwa ni wapangaji tuu katika minara inayomilikiwa na Helios Towers. Helios Towers inasimamia minara hiyo na hivyo kupunguza gharama kwa mitandao ya simu kwani zamani ilikuwa kila mtandao iliwabidi kumiliki na kusimamia minara yake.
Soma pia – Airtel wauza Minara yao ya Simu – Dalili nzuri au mbaya?
Kwa Tanzania minara ya kampuni hiyo inatumika kuwafikia wateja wa Tigo, Airtel, Vodacom na Halotel.
Chanzo: CNBCAfrika na vyanzo mbalimbali