Mapema mwezi wa sita tuliandika kuhusu uamuzi wa kampuni maarufu ya BlackBerry kuleta simu zinazotumia Android sokoni. Uamuzi huu kwa wengi ulipokelewa vizuri kwani tayari ingawa kampuni imeshatoa simu nyingi zenye mvuto katika miaka ya hivi karibuni hazikufanikiwa sana sokoni kwa sababu tayari watumiaji wengi wanataka programu endeshaji iliyoshiba katika eneo la apps mfano wa Android na iOS.

Picha za inayoonekana kuwa ni simu kutoka BlackBerry ikiwa inatumia toleo la programu endeshaji ya Android imesambaa mtandaoni kuanzia jana. Simu hiyo yenye eneo la kibodi (keyboard) imeanza kusambazwa na mtu mmoja maarufu katika kutoa taarifa za uhakika za kisiri kuhusu makampuni mbalimbali ya elektroniki hasa hasa kwenye masuala ya simu.

Je itakuja lini?
Simu hiyo inayofahamika kwa jana la BlackBerry Venice inategemewa kuingia sokoni ikifika mwishoni mwa mwaka huu na bei pia bado haijajulikana.
[socialpoll id=”2276589″]
Wengi wanategemea simu hiyo kufanikiwa kwani katika simu janja nyingi zilizopo sokoni kwa sasa bado hakuna simu tamu yenye kibodi, na hivyo inategemewa wengi ambao bado walikuwa na mapenzi ya simu kutoka BlackBerry watapata sababu nzuri ya kurudia kununua simu za kampuni hiyo.
Soma – Blackberry Kutoa Toleo La Simu Itakayotumia Android!?
Endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona na tutakutaarifu zaidi kuhusu ujio wa simu hii habari zikizidi kutufikia.
No Comment! Be the first one.