FACEBOOK ILIANZAJE? Yote ilianza kutoka kwa FACEMASH. Facemash ni mtangulizi kabla ya facebook au kwa maana nyingine facemash ilizaliwa kabla ya facebook. Mark Zuckerberg aliigundua na kuzalisha Facemash oktoba 28, 2003. Wakati alipozalisha Facemash alikua katika mwaka wake wa pili wa masomo katika chuo cha Harvard. Kazi ya tovuti hiyo ilikua ni kuwezesha kujua kama mtu ni mzuri ama sio mzuri (hot or not).
Tovuti ilihusisha kuweka picha mbili za wanafunzi ambapo watu wengine wangeweza kuwaona na kupiga kura yele wanemuana ni mzuri na yule mbaya. Mark Zuckerberg alipata mashtaka ya uvunjaji usalama (security breach) na uvujaji wa siri baada ya kuiba picha za wanafunzi wa chuo cha havard kwa kutumia kompyuta. Lengo la kuiba picha hizo lilikua ni kwa ajili ya kuzitumia katika tovuti ya Facemash. Tovuti ilifungiwa na uongozi wa Chuo cha Havard.
Katikati Ya Facemash & Facebook: TheFacebook
Baada ya Facemash, Mark Zuckerberg alianza kuandika ‘code’ zingine kwa ajili ya kufungua tovuti mpya. february 4, 2004 alifungua tovuti iliyoitwa TheFacebook. tovuti hii ilikua inapatikana kwa www.thefacebook.com lakini thefacebook kwa sasa ndio facebook tuu. mwaka 2005 kampuni liliondoa herufi ‘the’ katika mtandao huo na kubakiwa na www.facebook.com. Anuani ya facebook.com ilinunulia wa dola za kimarekani 200,000 mwaka huo.
Njia Nyingine Za Kuingia Katika Tovuti Ya Facebook
Unaweza ukawa unajua njia moja ya kuingia Facebook lakini ukweli ni kwamba unaweza ingia katika tovuti hiyo kwa kupitia njia nyingi tuu. Ndio kuna njia tatu za kuweza kuingia facebook. Ya kwanza ni ile maarufu ya www.facebook.com na ya pili ni ile ya zamani ya www.thefacebook.com na ya tatu ambayo ipo kwa ufupi pia ni www.fb.com , wale wavivu wataipenda hii ya tatu (Haa!)
Ukiongeza namba 4 Mwishoni Mwa Tovuti Itakupeleka Katika Wall Ya Mark Zuckerberg
Ukweli mwingine wa kuvutia ni huu. Kama unataka kutembelea profile mtu anaeimiliki Facebook basi inakubidi uongeze namba 4 mwishoni mwa tovuti hivyo, yaani www.facebook.com/4 ukisha bonyeza Go/Enter utaona 4 inabadilika na kujiandika Zuck, yaani www.facebook.com/zuck. Hili ni jina fupi alilolipa Profile lake lakini hata hivyo hatuna uhakika kwanini kalipa profile lake namba 4 kama nyia rahisi ya kumfikia.
Ili kutembelea Profile za Chris Hughes na Dustin Moskovitz ma CO wa Facebook inakubidi uongeze namba 5 na 6 mwishoni mwa www.facebook.com
Facebook Wanalipa Dola 500 Kama Utaona Mdudu (Bug) Katika Mtandao Wao
Ndio Ni kweli Facebook wana programu inayoitwa ‘Bug Bounty program’ ambayo inahusika na kulipa watu amabao watakuta kirusi/mdudu (bug) katika tovuti hiyo. watu wanasema dola 500 ni kiasi cha juu lakini ukweli ni kwamba hicho ni kiasi cha chini cha program hiyo ya Bug Bounty program. Facebook ilishamlipa mtu mmoja dola 500 kwa ripoti nzuri aliyoiandaa, na pia kwa kila mdudu mmoja atakaepatikana Facebook italipa dola 500.
Kutaka kujua zaidi kuhusu Bug Bounty program Bofya Hapa
Mpaka sasa Facebook ndio mtandao unaoongoza kwa watumiaji duniani kote. Ningependa Kusikia kutoka kwako, coment yako ni muhimu sana. Pia Tembelea kurasa Zetu Za Facebook, Twitter na Instagram
No Comment! Be the first one.