Tableti ya HTC A101 ni tableti mpya mjini. Kampuni ya HTC kuna kipindi ilikua imeshika chati kwenye soko la simu ikishindana na Samsung.
HTC bado hawapo nyuma, wametambulisha tabiti mpya huku wakiwa na mipango kadhaa, moja kati ya mipango yao juu ya tabiti hii ni kwamba imeandaliwa mahususi kwa soko la afrika.
Tabiti hii inakuja kwa jina la HTC A101 na inakua na mfumo wa Android huku kioo chake kikiwa na ukuwa wa inchi 10.1
Toleo hili linakua ni kama muendelezo tuu wa tabiti ya HTC A100 ambayo ilizinduliwa mwaka uliopita. Tabiti hizi zimejikata sana katika masoko ya simu ambayo bado yanakuwa pengine ndio maana hata hazipigiwi kelele sana.
Pengine unaweza ukawa unashangaa kwanini bado HTC kama kampuni inapambana katika kuhakikisha kuwa inawaletea bidhaa wateja wake licha ya kuwa imeporomoka sana katika soko sio?
Kumbuka pengine HTC ndio kampuni ya kwanza kabisa kuanza kutengeneza na kuuza simu inayotumia mfumo wa Android.
Tabiti hii inakuja na prosesa ya Unisoc T618, GB8 za RAM huku ujazo uhidfadhi ukiwa ni GB128, lakini pia unaweza kuongeza ujazo uhifadhi kwa kuongeza memori kadi ya nje.
Ina kamera mbili kama vifaa vingi siku hizi, kamera ya kwanza ikiwa na MP16 wakati ile ambayo inapiga picha kwa ukubwa (eneo kubwa) zaidi inakuaja na 2MP. Kamera yake ya mbele ikiwa na MP5.
Kingine kikubwa ni kwamba ina uwezo wa kutoa loki kwa utambuzi wa sura, inakuja na tundu la spika za masikio na pia betri lake lina ujazo wa 7,000mAh.
Kinachowashangaza wengi sio HTC kuleta kifaa hichi bali ni aina hii ya uingizwaji sokoni kwa bidhaa hii yaaani hakuna promo (matagazo) kubwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment hapo chini, je wewe unaweza kutumia bidhaa hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.