Kwa kutumia akili bandia (AI) ni wazi kwamba vifaa vyetu vya kieletroniki vinaweza kuongea sio? Lakini hebu fikiria kwa sasa Apple (iPhone Na iPad) wanakuja na uongeaji huo lakini ambao unatumia kabisa sauti yako.
Uwezo huu katika iPhone unatarajiwa kuja rasmi kabla ya mwaka huu kuisha. Kwa sasa kumbuka ni kwamba kwa kutumia siri utaweza chagua sauti mbalimbali (za mwanamke/mwanaume) ambazo sio za kwako –katika matumizi ya kawaida kabisa.
Ni ni mara kwa mara kwa kutumia maroboti yanayotumia AI katika vifaa vyetu kama vile Siri –kutoka Apple—n.k unaweza kuyaamuru kufanya vitu mbalimbali kama vile kukusomea meseji n.k…….. sasa pata picha sauti hiyo ikiwa ni yako.
Sasa Kubwa Zaidi Ni Hili Hapa …………….
Uwezo huu utakua unapatikana katika eneo la misaada ya ziada yaani Assistive Access na Live Speech ambayo yatakua yanapatikana katika eneo la Accessibility ndani ya Settings.
Kazi Kubwa Ya Vipengele Hivi.
𝗟𝗶𝘃𝗲 𝗦𝗽𝗲𝗲𝗰𝗵:
Kwa mtu ambayo labda hajui/amepoteza uwezo wa kuzungumza itamsaidia kuweza kuandika ujumbe ambao anataka kuuzungumza na mtu wa upande wa pili ataona ujumbe huo huku simu ya sauti (Voice Call) bado inaendelea.
Hili ni jambo zuri sababu kuna baadhi ya nyakati zinatokea uko kwenye simu lakini kuna vitu unashindwa zungumza na upande wa pili kwa sababu tuu ya mazingira ya hapo yanakubana.
𝗔𝘀𝘀𝗶𝘀𝘁𝗶𝘃𝗲 𝗔𝗰𝗰𝗲𝘀𝘀:
Hii itakua ni rafiki kwa watu ambao wana matatizo ya macho kwa maana ya kwamba mfumo mzima wa simu utakua na uwezo wa kukuza icons, buttons na vile vile kuzingatia kuweka muonekano ambao uko rahisi kuonekana.
Sehemu ambazo zitaguswa katika Camera, Photo, Music, Calls, na Messages kwa kuanzia, lakini kwa baadae labda kutakua na uwezo wa kuongezea App zingine.
…..
Jinsi ya kufanikisha kipengele cha Live Speech ni kwamba itambidi mwenye simu asome kwa sauti maneno machache ambayo yatatokea katika uso wa iPhonea au iPad yake ila kifaa hicho kinase vizuri sauti yako na kuielewa
Baada ya hapo mtu anaweza kuandika maneno ambayo yanaweza yakachukua hata dk 15 katika yakiwa yanasikilizwa na mlengwa… hii ni nzuri sana kwa watu wenye matatizo kidogo katika swala zima la uongeaji mfano wenye saratani ya oo
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani utaanza kutumia kipengele hiki kikija (pengine kitakuja na iOS 17). Niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.