CAPTCHA ni kitu gani? Hivi wakati unazunguka zunguka huko mtandoani hujawahi kutana na swali linaolouliza Are You A Robot?..
… ukishaona swali kama hilo huwa kuna vitu unatakiwa kufanya ili kwenda katika ukurasa ambao ulikua umeutegemea…na ili kupita hapo ilibidi ujaze maneno na namba ambayo umepewa juu yake.

CAPTCHA ni njia moja wapo ambayo inatumika katika kutofautisha kompyuta (kama vile roboti) na wanadamu huko mtandaoni
Saa zingine inabidi ujibu maswali ambayo yameulizwa kwa usahihi kabisa ili kuweza kupita na kwenda katika ukurasa ulioutegemea.
Kumbuka kwa haraka haraka jambo hili huwa kuna namna linachosha na asilimia kubwa unaweza ukawa unajiuliza kwanini mtandao unaweza kukuuliza hivyo? Kwani nyendo zako mtandaoni hazionekani kama wewe sio roboti???
Jambo hili kwa iOS na MacOs litakua limebadilika kwani kwa kutumia kipengele kipya wanachokiita “automatic verification” kutumia vifaa hivyo ya Apple CAPTCHA hizo zitakua zinapitwa ki automatiki.

Kinachotokea hapa ni kwamba teknolojia hii itaruhusu mitandao mbali mbali kujiaminisha kwamba wewe sio roboti bila wewe kuweza kufanya chochote.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani jambo hili litangia mpaka kwa aina nyingine ya simu kama vile zile za Android?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.