Kama hujui kuhusina na hili basi ondoa shaka. Ni historia fulani ambayo tuu inaelezea kila kitu juu ya jina hilo.
Kwa karne hii ya 21 Bluetooth ni njia ya karibu sana na ya haraka ya kuweza kutuma na kuhamisha mafaili kutoka kifaa kimoja hadi kingine. Licha ya kuijua Bluetooth na kazi yake inayofanya hivi ushawahi kujiuliza kwa nini iliitwaga hivyo na sio kitu kingine?
Stori ni ndefu kidogo ila ngoja niifupishe.. naomba nikupeleke mwaka 1966 ambapo Jim Kardach (mmoja kati ya waanzilishi wa kwanza kabisa wa teknolojia ya Bluetooth) alikuja na hilo jina. Jina lilipatikana wakati walipokuwa wakipiga stori za kihistoria.
Katika stori hizo mara jina la mfalme Harald “Bluetooth” Gormsson likajitokeza. Mfalme huyo alipata umaarufu wake huko Denmark na Norway baada ya kuunganisha makabila tofauti tofauti katika nchi hizo mnamo karne ya 10.
Aliweza kuunganisha baadhi ya makabila ya nchi hizo mbili na kuyafanya yawe na maadili ya dini ya kikiristo.
Lakini bado kuna vyanzo vingine vilienda ndani zaidi na kusema kuwa mfalme huyo, Harald alikuwa na meno mabaya ambayo yalikua na ubluu bluu ndani yake. Hii pia inaweza ikaonyesha sababu ya watu kumuita Bluetooth.

Kutoka na historia hiyo ya mfalme Harald ya kuweza kuunganisha watu karibu na ukiangalia teknolojia hii kazi yake kubwa ni kuunganisha na kubadilishana mafaili mbalimbali ndipo hapo Bw. Kardach alipoona jina la ‘Bluetooth’ linafaa kabisa.