Leo tutakueleza jinsi ya kuweza kufungua mitandao maarufu ambayo inaweza kufunguka/kutumika kwa watu waliokatika nchi flani tu. Hii mara nyingi inakuwa katika mitandao ambayo baadhi ya huduma zao kama vile muziki au video wanajikuta wamebanwa kisheria au kimikatika kuonesha data/huduma husika kwa nchi zingine.
Je umeshakutana na ukurasa wa mtandao unasema kitu kama hiki?
Pia suala hili linaweza kuja ata pale unapotaka kuangalia baadhi ya video katika akaunti ya YouTube;
Njia rahisi ya kushinda suala hili ni kupitia kutumia programu moja inayeweza kufanya kazi kama kiprogramu cha nyongeza (extensions/plugins) kwenye Chrome au Firefox inayofahamika kwa jina la Hola. Programu hii inapatikana pia kwenye Android na itakuwezesha kutumia apps zinazonyima baadhi ya huduma zake kwa watu walio katika nchi flani.
Kwa ufupi Hola itakupa uwezo wa wewe kuchagua unataka kutambulika kama mtumiaji kutoka nchi gani, utaweza kuchagua na kubadilisha kwenda nchi yeyote utakayoitaka yote ni ili kukuwezesha kuweza kupata huduma husika.
Kwenye Android utafungua app hiyo na kuchagua app unayotaka idanganya uhalisia wa nchi uliyopo, kisha ndiyo utafukua app husika.
Kupakua bofya sehemu husika Android | Chrome | Kwa ajili ya iOS, Windows, Firefox na Mac <Bofya Hapa>
No Comment! Be the first one.