Kampuni mbalimbali zinajitahidi kutoa kompyuta ambazo zinaleta ushindani na hasa wakiangazia zaidi uwezo, umbo na hata uzito wa kifaa husika, Honor ambao wamekuwa wakitoa simu janja lakini sasa wametoa kompyuta yao ya kwanza.
Simu janja zimeonekana zikiweza kufanya mengi tu ambayo hayahutaji tena utumie kompyuta ili kazi ifanyike tofauti na huko nyuma ilibidi utumie kompyuta ili mambo yaende sawa. Hata hivyo, bado kwa kiasi kikubwa tu kompyuta zina nafasi kubwa katika kufanikisha vitu vingi ambavyo si rahisi kuvifanya kwa kutumia simu.
Honor MagicBook-Kompyuta mpakato ya kwanza kutoka Honor ambapo ni jina la bidhaa zilizo chini ya Huawei.
Uchambuzi kuhusu Honor MagicBook.
1. Uwezo
Kompyuta yoyote ya kisasa ni muhimu sana iwe imejitosheleza vilivyo kwenye upande wa prosesa, ubora wa picha (graphics), RAM, diski uhifadhi, betri (uwezo wa kutunza chaji), n.k ili kuweza kuvutia wateja na kwenda kukata kiu ya yule ambae ataenda kuitumia.
Prosesa. Honor MagicBook zipo za aina mbili tofauti; moja ni kizazi cha 8 cha prosesa Intel Core i7 na Core i5. RAM ya kwenye kompyuta hii ni GB 8. Kuhusu kasi kwenye kompyuta hii sio suala la kuhofia kwa sababu kama kompyuta ikiwa na RAM kuanzia GB 8 na prosesa iwe core i5 au i7 basi unatakiwa ufurahi tu kuwa una kompyuta nzuri.
Ubora wa picha (graphics). Kama mtu anajua vizuri kuchagua kompyuta nzuri basi lazima atakuwa makini sana kutaka kujua kompyuta anayotaka kuinunua ina nini kizuri kwenye upande wa picha. Uzuri ni kwamba kwenye Honor MagicBook si haba, ina 2GB Nvidia GeForce GeForce MX150. Kiwango cha ubora wa picha ni 1920x1080p.
Uwezo wa kukaa na chaji/betri. Moja ya kipengele ambacho mtu atataka kujua pale anapotaka kununua kompyuta ni uwezo wa kompyuta mpakato kutunza chaji. Basi kwa Honor MagicBook kipengele hiki wakitendea haki ya hali ya juu sana kwani betri yake ina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa saa 12. Inachaji kutoka (0-70)% ndani ya saa moja tu, nguvu yake ya betri ni 57.4Wh.
Diski uhifadhi. Hiki ni kipengele kingine ambacho wengi wetu huwa tunakizingatia sana na hasa kutokana na matumizi ya mtu mwenyewe. Honor MagicBook ina 256GB SSD na kumbuka kuwa kompyuta ambayo inatumia diski uhifadhi aina ya SSD ni bora zaidi kuliko ile inayotumia HDD. Kutaka kujua kwanini na kiundani zaidi BOFYA HAPA.
Umbo la Honor MagicBook linafanana sana na kompyuta za Apple kutoka familia ya MacBook lakini sasa tofauti yake inakuja kwenye vipimo halisi; kompyuta ya kwanza kutoka Honor ni inchi 14 ikiwa na upana wa 5.2mm. Uzito wake ni Kg 1.47.
Honor MagicBook inaweza kufananishwa na Apple kwa macho ya karibu lakini kompyuta za MacBook inatofautiana kwa mengi tu mbali na kufanana kiumbo kwa kiasi kikubwa.
3. Bei na kuanza kupatikana
Honor MagicBook imekuvutia? Basi ni vyema ukafahamu kuwa ile ambayo ni core i5 inauzwa kwa $800|Tsh. 1,800,000 na core i7 inapatikana kwa $900|Tsh. 2,025,000. Bei zilizotajwa ni iwapo tu utanunulia ughaibuni. Tayari imezinduliwa lakini itaanza kuuzwa Aprili 23.
4. Mengineyo
Honor MagicBook ina USB Type-A 3.0, USB Type-A 2.0, an HDMI port, 3.5mm headphone jack, spika 4, mic 2, inatumia ulinzi wa alama ya kidole. Pia, kompyuta hiyo ina programu tumishi iitwayo Magic-Link inayowezesha kuhamisha/kupokea vitu mafaili kati ya Huawei na kompyuta yenyewe. Ina feni moja tu inayopooza prosesa pamoja na graphics kadi kupita sehemu tatu. Inapatikana katika rangi ya Kahawia, Udhurungi na Fedha pis kioo chake ni cha mguso.
Kompyuta zipo nyingi sokoni ila kwa sifa za Honor MagicBook inabidi ujipange vyema kuweza kuinunua lakini kiujumla ni kompyuta nzuri na yenye uwezo wa hali ya juu. Wewe je, unaizungumziaje kompyuta hii?
Vyanzo: Gadgets 360, BETA News
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
One Comment
Comments are closed.