Simu ya HTC One inayotumia Android imepata sifa ya kuwa simu bora zaidi kiuwezo kwa maoni ya wateja na watafiti wa mambo. Wakati HTC One inatoka mwezi wa pili mwaka 2013 tuliandika makala kuhusu sifa zake (Soma hapa -> HTC ONE: Simu Yenye Mvuto Na Uwezo Wa Hali Ya Juu!), HTC One imekuwa ni moja ya simu zilizofanya vizuri zaidi kutoka HTC, kwa mwaka 2013 zaidi ya simu milioni 6.3 za toleo hilo ziliuzwa. Kutokana na mafanikio ya simu hiyo mwezi wa tatu mwaka huu HTC wakaja na HTC One M8 ambayo imefanya vizuri sokoni lakini HTC hawajatoa taarifa zaidi ya mauzo ya simu hiyo.
Na sasa HTC wanatengeneza toleo la HTC One M8 linalokuja na programu ya uendeshaji ya Windows Phone 8.1. Hili litakuwa jambo la kimfanikio kwa kampuni ya Microsoft kwani HTC One M8 ni simu yenye uwezo mkubwa wa kiundeshaji na pia ni simu yenye muonekano na mvuto wa kipekee. Hakuna kitu cha ndani cha kiufundi kilichobadilishwa kwenye toleo hili, sifa zote za kiuwezo zinafanana na zile za toleo la mwezi wa tatu linalotumia Android.
Kama toleo hili litafanya vizuri sokoni basi mafanikio yatakuwa kwa wote Microsoft na kwa HTC. Kwa kipindi cha zaidi ya mwaka sasa Microsoft wamejaribu kuipigania kimatangazo programu ya Windows na simu zinazotumia programu hiyo kama ni programu yenye uwezo mkubwa na ubora wa kulinganishwa na Android na iOS. Mafanikio ya simu hii ni muhimu kwa kampuni zote mbili, wakati Microsoft inapigania mafanikio ya programu ya Windows, HTC inajitaidi kurudisha mafanikio ya kimapato kwani kwa miaka miwili mfululizo mapato yao hayajakuwa mazuri sana.
Sifa/Uwezo wa HTC One M8
Ukubwa: 5.8 x 2.7 x 0.37 (inchi)
Ukubwa wa Kioo: 5.1 inchi, 1,920×1,080 pixels; 431ppi
Programu Uendeshaji (OS): Windows Phone 8.1
Inauwezo wa 4G LTE na Bluetooth 4
Kamera ya Nyuma:“Ultrapixel”; 1080p HD video
Kamera ya Mbele: 5-megapixel; 1080p HD
Processor: 2.3GHz quad-core Snapdragon 801
Uwezo wa Betri: 2,600mAh
Uwezo wa Uhifadhi: 32GB (Pia unauwezo wa kuongeza kupitia kadi)
RAM 2GB
Rangi: Kijivu
Bei yake kwa sasa haijatolewa, ila bei ya toleo linalotumia Android ni dollar 600 za kimarekani (Takribani Tsh 996,900/=), na kuna uwezekano mkubwa bei ya toleo la Windows kutozidi bei hiyo.
No Comment! Be the first one.