Hivi karibuni Huawei ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Duka lake la programu la AppGallery litakalokuwa kwenye simu zake za Huawei. Taarifa kutoka Huawei zinasema AppGallery ya sasa limekuwa duka kubwa la tatu duniani baada ya Android(Play store) na Apple (App store).
AppGallery imekuja baada ya zuio la Marekani kwa Huawei kutotumia App za nchi hiyo ikiwemo Play Store inayobeba programu nyingi maarufu.
Tangu uzinduzi wa AppGallery Huawei imekuwa ikiwavutia watengenezaji wa program mbalimbali duniani kuweza kuweka programu zao kwenye Duka hilo. Aidha watumiaji wa AppGallery wamekuwa wakiongezeka kufikia milioni 400 kwa mwezi na kukiwa na zaidi programu 55,000 ndani ya AppGallery.
Huduma ya AppGallery inapatikana katika nchi 170 na ikishirikiana na watengenezaji wa App kutoka Asia, Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, na Amerika ya Kusini.

Kampuni hiyo pia ilitangaza kuwa itakuwa na uzinduzi wa “Quick App”, huduma ambayo itawawezesha watumiaji kujaribu/kutumia programu bila ya kuwa na haja ya kudownload na kuinstall. Hii itasaidia kwa simu zenye uhifadhi mdogo.
Taratibu Huawei wanaanza kujijenga kuepukana na ukiritimba wa utawala wa Marekani katika Teknolojia.
Unaweza kupakuwa na kuweka AppGallery katika simu yako yoyote ya mfumo wa android kwenye Link hapo chini.