Huawei ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika Nyanja nzima ya sayansi na teknolojia, mara kwa mara kampuni imekua ilileta teknolojia kubwa ambazo huwa zinawashangaza wengi.
Kuna kupindi Huawei kupitia sekta ya kutengeneza na kuuza simu janja iliweka rekodi mara baada ya kupita baadhi ya chapa kubwa duniani (kama vile iPhone) kwa mauzo ya simu huko china.
Licha ya kuwa na teknolojia kubwa lakini bado kuna mambo mambo yalitokea na kuipelekea kampuni kuzuiwa baadhi ya bidhaa zake (kama vile simu janja) katika baadhi ya maeneo –soma Zaidi >>HAPA<<
Hivi karibuni bila kutegemewa Huawei imeachia simu janja babkubwa ikiwa na sifa za tofauti kabisa na simu janja zingine.
Ikiwa na sifa kede kede za kipekee kama uwezo wake mkubwa kaitka chip na ufanisi, simu janja hiyo ni Huawei Mate 60 Pro.
Hii inawapelekea wengi kuona kabisa kwa jicho la tatu kwamba kampuni hiyo kidogo kidogo itakau na mpango wa kutaka kurudi katika soko la simu janja la dunia.
Ni wazi kwamba kampuni ya Huawei kwa chini chini imeanza kaundaa mifumo na timu nzima za masoko kwa soko la dunia.
Ni wazi kwamba Huawei mwezi wa tano ilizingua simu janja za Huawei P60 Pro na hata Huawei Mate X3 ikiwa ya kijikunja (Fold) na baadhi ya masoko kama vile ujerumani, falme za kiarabu, Malaysia na hata mexico.
Ukiachana na hayo kingine ni kwamba kwa mwaka huu pia kampuni inategemewa kuzindua simu janja nyingine huko spain.
Ni wazi kwamba kwa takribani ya kipindi cha miaka mitatu Huawei imekua kimya katika kutoa simu katika masoko ya kimataifa lakini hii inaonekana dhahiri kwamba inabadilika.
Mara tuu baada ya kampuni kuja na toleo la Huawei Mate 60 inaonyesha kabisa kwa mwaka huu pekee itafika mpaka mauzo ya milioni 10 mpaka 12.
Na kingine wataalam wa mambo wanasema kwamba kulingana na mambo yanavyoenda namba hiyo inaweza kusogea mpaka kufikia milioni 15 mpaka 17.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani kampuni itatoboa katika soko la dunia kama zamani?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.