Huawei licha ya kupitia changamoto nyingi katika soko miaka kadhaa iliyopita bado wanahakikisha kuwa wateja wake wanapata bidhaa kutoka kwao.
Huawei ni moja kati ya makampuni makubwa sana yanayojihusisha na maswala ya kutengeneza na kuuza simu na bila kuachana na aina nyingine ya teknolojia.

Kupitia katika tovuti yake imetangaza simu nyingine ambayo inakwenda kwa jina la Huawei Nova Y61 na hii itakua ni mwendelezo wa Huawei Nova Y60 ambayo ilitoka mwaka jana.
Sifa Zake.
Umbo lake ni zuri na ni jembamba vile vile sehemu yake ya kamera imefanana kama ile ya iPhone katika matoleo ya Pro.
Kamera zake ni tatu huku ile kubwa (ya nyuma) ikiwa na 50MP, huku zingine za nyuma zikiwa ni 2MP ile ya macro na 2MP ya depth sense, huku kamera ya mbele ikiwa ni 5MP.

Inakuja katika jumba la plastic (kulingana na fununu) huku vipimo vyake vikiwa ni 164.28 x 75.8 x 8.94mm na inakuja katika rangi tatu, bluu, kijani na nyeusi.
Kioo chake ni cha inchi 6.52 huku kikiwa ni cha HD+ na prosesa yake inaendeshwa na chip ambayo haijawekwa wazi ila ina uwezo wa Octa-core.

Kwa soko la bara la asia simu hii itapatikana ikiwa na RAM 6GB na 64GB za ujazo uhifadhi wa ndani huku masoko mengine yakiwa na 4GB za RAM naGM Ujazo uhifadhi wa ndani.
Kingine kizuri ni kwamba kwa baadhi ya maeneo itauzwa ikiwa inaruhusu laini mbili wakati maeneo mengine itakua ikiuzwa ikiwa na sehemu ya laini moja tuu.
Uwezo wake wa betri ni 5,000mAh huku ikiwa na uwezo wa kuruhusu chaji wa muda mchache (fast charging).

Kampuni ya Huawei bado ina matoleo mazuri sana ya simu ambayo katika soko yanasimama kama shindani kwa makampuni mengine ya simu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Unadhani simu hii italeta ushindani kwa makampuni mengine ya simu kulingana na sifa hizo tajwa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.