Huawei ambao wamekuwa wakisikika kuhusu programu yao endeshi kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Uchina imeweka wazi tarehe rasmi ya ujio wa HarmonyOS.
Habari kuhusu ujio wa HarmonyOS zimevuma kwa sana katika miezi ya karibuni lakini sasa tarehe rasmi ya ujio programu endeshi imewekwa wazi ambapo itafanyika hafla ya uzindunzi.
Kitakachofanyika kwenye uzinduzi wa programu endeshi ya Huawei
SIku hiyo ya Juni 2 2021 pamoja na utambulisho wa programu endeshi pia simu janja MatePad Pro 2 na Huawei Watch 3 ambazo zote zitakuwa na hicho cha kwao wenyewe.
Baada ya uzinduzi wa HarmonyOS kuna simu janja ambazo zimewekwa kwenyw mpango wa kuruhusu wanazimiliki kuweza kushusha toleo hilo na kuanza kutumia’ kwa lugha rahisi kutoka kwenye Android na kuhamia HarmonyOS. Rununu ambazo zipo kwenye mpango ni Mate 40, Mate 40 Pro, Mate 40 Pro+, Mate 40 RS, Mate X2, Nova 8, Nova 8 Pro na MatePad Pro.
Fununu zinasema HarmonyOS na Android ni kama mapacha wasiofanana kutokana na jinsi ambavyo inaonekana na hata vipengele vyake ndani lakini kwa sasa inatubidi tuwe wavumilivu hadi Juni 2 2021 tutakapoweza kufahamu kila kitu kinagaubaga.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
4 Comments