Huawei wametoa simu rununu ambayo mtangulizi wake (Huawei Mate 20) alionekana kufanya vyema kwenye soko la ushindani na sasa wahusika wameleta toleo jingine likifahamika kama Huawei Mate 20 Lite.
Simu yenyewe ina majina mawili ambayo unaeza ukafikiri ni bidhaa mbil tofauti lakini la hasha! Jina la kwanza ni Huawei Maimang 7 lakini ambalo linafahamika kiurahisi ni Huawei Mate 20 Lite.

Uzinduzi wa simu yenyewe ulifanyika nchini Uchina na sifa za Huawei Maimang 7 ni kama ifuatavyo:-
Kipengele |
Maelezo |
Muonekano/Kioo | Kioo kina urefu wa inchi 6.3 (1080×2340 pixels), muonekano ang’avu lakini pia ina umbo la herufi ya “V” kwenye uso wa juu. |
Kipuri mama/Programu endeshi | Kirin 710 ndio iliyowekwa prosesa na Mali-G51 MP4 GPU kufanya vitu vionekane vizuri kabisa kwenye simu.Programu endeshi iliyopo ni Android 8.1 Oreo. |
Mawasiliano/Kadi za simu | Simu hiyo ina 4G, VoLTE na inaitumia kadi mbili za simu. |
RAM/Diski uhifadhi | GB 6 upande wa RAM na GB 64 kwenye memori ya ndani lakini unaweza ukaweka memori ya ziada ya mpaka GB 256. |
Kamera | Kamera mbili za nyuma zenye MP 20+ 2MP pamoja na flash, kamera za upande wa pili nazo ni mbili MP 24+2MP. |
Betri | Nguvu ya betri ni 3750mAh ikiwa na teknolojia ya kuchaji haraka. |
Mengineyo | Uzito wake ni gramu 172, ina Bluetooth 4.2 LE, GPS + GLONASS, USB Type C na Wi-Fi 802.11 ac. |
Tayari imeshaingia sokoni na bei yake ni $350|805,000 kwa ughaibuni.
Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena