Huawei ni moja kati ya makampuni makubwa sana kwenye swala la teknolojia. Vifaa vyake vingi ambavyo vinaingia katika soko moja kwa moja huwa vinafanya vizuri.
Kwa sasa kampuni imetambulisha spika za masikio –zile ambazo hazina waya—ambazo wamezipa jina la Huawei FreeBuds 5.
Spika hizi zimewaaacha wengi mdomo wazi kwa sasabu ya muonekano wako na hapo ni ukiachia mbali na sifa zake za undani.
Muonekano wake ni mithili ya tone –la maji—ambapo kwa kiasi kikubwa inaweza isionekane kama zile spika zingine za masikio ambazo tumezizoea.
Kingine kizuri ambacho Huawei umeeleza ni kwamba imefanya muonekano huu makusudi kabisa ili mradi spika hizo kukaa vizuri zikiwa sikioni kwa mtumiaji.
Unaambiwa FreeBud 5 muundo wake wa betri, spika na hata ule utambi wake wa ndani kabisa ziko mbali mbali kwa kiasi kwamba inasaidia sauti kutoko vizuri.
Licha ya sauti kutoka vizuri kingine sababu ya teknolojia ya kuchuja sauti na kuzuia sauti za nje kuingia ndani ya maskio ni kwamba hata betri lake linawahi kujaa chaji na kingine unaweza litumia mpaka masaa 30.
Huawei wenyewe wanajisifia wanasema kwamba kwa muda wa dakika tano tuu utapata ongezeko la masaa mawili ya kutumia spika hizo.
Spika hizo kutoka Huawei pia zinatumika hata katika simu za Android na iPhone na zinakuja na teknolojia ya Hi-Res Audio Wireless certified (96 kHz/24 bit) ambayo iko vizuri kwenye upande wa sauti.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niiandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani spika hizi zitazipiku zile ambazo ziko sokoni kwa sasa mfano kutoka kwa Apple na Samsung?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.