Karibu mara zote ambazo Huawei wanazindua bidhaa zao basi huwa wanafanya mkutano ambao unahusisha kile ambacho wanataka kukionyesha rasmi kwa ulimwengu lakini mambo ni tofauti kwa MediaPad M5 lite.
Tunafahamu simu/tabiti mbalimbali ambazo zimebemba nemo ya Huawei na kuhusu kasi ya utoaji wa tabiti sio wa kasi kulinganisha na simu rununu. Siku kadhaa zilizopita kampuni hiyo ilitoa MediaPad M5 lite bila ya taarifa rasmi (kimyakimya).
Bidhaa hiyo inabeba sifa kadha wa kadha kwa wale ambao tunapenda kutumia tabiti katika kufanya mawasiliano kwa njia mbalimbali. Sifa zake ni kama ifuatavyo:-
Kipuri mama+Umbo.
Muonekano wake ni wa kioo chenye urefu wa inchi 10.1, uwiano wa 16:10 (1920 x 1200 pixel), lakini pia ikiwa na spika nne (4). Kuhusu kile kinachobeba mfumo mzima wa bidhaa husika kwa lugha rahisi kipuri mama ni Kirin 659 SoC.
RAM+Diski uhifadhi.
MediaPad M5 Lite impo katika matoleo mawili tofauti; moja ikiwa na RAM GB 3/32GB memori ya ndani, nyingine ikiwa na RAM GB 4 na GB 64 diski uhifadhi.
Bertri+Programu endeshi
Tabiti zinaweza kutumiaka kufanikisha mambo mbalimbali na hivyo kuwa na ulazima wa kukaa na chaji kwa muda mrefu. MediaPad M5 Lite ina betri yenye 7500mAh lakini pia ikiwa na teknolojia ya kuchaji haraka. Bidhaa hiyo imewekwa toleo la Android 8.0 maarufu kama Oreo.
Usalama wa macho.
Matumizi ya vifaa vya kidijiti vinachangia matatizo ya macho mathalani uwoni hafifu, macho kuuma, n.k lakini kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Huawei wameeleza kuwa tabiti MediaPad M5 Lite itatoa ujumbe iwapo mtu anayeitumia ameisogelea kwa karibu kioo chake.
Rangi, Bei na Mengineyo.
idhaa hiyo inakuja katika rangi ya Dhahabu na Kahawia lakini pia ikiwa na kalamu ya kidijiti kwa ajili ya kusaidia kuperuzi huku na kule, kuchora, n.k. Bei yake bado haijawekwa wazi.
Tujiapnge kuweza kununua bidhaa hiyo iwapo wewe ni mpenzi wa tabiti katika matumizi yako ya kila siku.
Vyanzo: Huawei, GSMArena