Huawei yashikwa kwa picha Feki. Siku chache zilizopita kampuni ya simu za mkononi ya Huawei ilichapisha picha kadhaa kama kampeni ya utambulisho (teaser campaign) kwa ajili ya ujio wa simu yao mpya ya Huawei P30 Pro.
Simu hiyo ya P30 Pro yenye kamera nne inatarajiwa kuzinduliwa wiki mbili zijazo, picha walizoziweka kuonesha ubora wa kamera katika simu hiyo zimebainika hazijapigwa na kamera ya simu hiyo.
Lakini imebainika kwamba picha walizoweka hazikupigwa na kamera ya simu hiyo ya P30 Pro bali kwa kamera halisi za DSLR.


Picha hizo ambazo waliziweka kwenye mtandao wa Weibo ili kuonesha uwezo wa kamera kwenye simu hiyo pamoja na uwezo wa kuvuta picha mara 7, imekuja kufahamika kwamba Huawei walinunua leseni ya picha hizo kutoka kwenye mtandao wa Getty Images.
Na kuzitumia kama teaser campaign kwa ajili ya simu yao hiyo mpya ya P30 Pro, wakiwa na lengo la kuwaaminisha watu kwamba picha zimepigwa na simu hiyo kumbe ni kamera ya DSLR.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Huawei kutumia picha ambazo hazijapigwa na kamera za simu zake bali kamera za kawaida za ubora wa juu.
Mara ya mwisho tukio kama hili walilifanya Agosti 2018 kwa simu ya Huawei Nova 3.
Wenyewe wamejitetea wakisema lengo la picha hizo kutumika haikuwa kusema ya kwamba picha hizo zimepigwa na Huawei P30 Pro. Ila waandishi wengi wanaamini wamekuja kujitetea hivyo baada ya kuona uongo huo kutambuliwa na wengi.