Huduma ya ulipaji matibabu ya Safaricom, M-Tiba imetambuliwa ulimwenguni kama teknolojia inayobadilisha maisha ya wananchi wa Kenya kwa kurahisiha jinsi ya kupata huduma za afya.
Huduma hiyo imeungana na huduma zingine zilizotambuliwa ulimwenguni kama vile Twitter, Spotify na Google ambazo zimebadilisha maisha katika jamii. Lakini M-Tiba ni nini? M-Tiba ni programu tumishi/huduma inayomuwezesha wananchi kulipia huduma za matibabu au kununua madawa hospitalini kwa kupitia M-Pesa.
Tangu kuanzishwa kwa M-Tiba mwaka 2016 imeweza kutumiwa na watu zaidi ya milioni moja huku watoa huduma za afya 700 wanakubali kupokea malipo/muamala uliofanyika kupitia M-Tiba.
Kwa lugha ya kiteknolojia unaweza kusema unatembea na pesa katika mfumo wa kidijitali ambapo unaweza kufanikisha kupata huduma za afya kwa haraka zaidi.
Huduma hiyo inayotolewa kwa njia ya programu ilitambuliwa na World Economic Forum (WEF) na M-Akiba ni miongoni mwa kampuni tatu kutoka barani Afrika ambazo zilitambuliwa mwaka huu.
Huduma ya M-Tiba inapatikana mpaka pale mtu anakapokuwa amejiunga na huduma hiyo hivyo haimaanishi kuwa ukiwa umejisajili na M-Pesa ya Kenya moja kwa moja unakuwa tayari umeshajiunga na huduma hiyo ya M-Tiba.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.