Kuzuiwa kwa huduma ya Netflix Indonesia itakuwa ni pigo kubwa kwa Netflix toka ilipotangaza kuanza kupatikana duniani kote. Soko la Indonesia ni kubwa na si la kulikosa.
Kampuni ya mawasiliano (mtandao wa simu na huduma ya intaneti) inayomilikiwa na serikali ya Indonesia imeanza kuzuia Netflix nchini humo kwa sababu maudhui yanaoyooneshwa ni yale yenye kuchochea vurugu na pia au yale ambayo yamelengwa kwa watu wazima, pia kampuni hiyo imesema Netflix bado haina kibali halali kwa ajiri ya kufanya kazi Indonesia.
Indonesia ni nchi ya nne kwa wingi wa watu duniani, na iwapo zuio hili halitaondolewa basi kutakuwa na madhara makubwa kwa mtandao wa Netflix ambao uliweka wazi mpango wake wa kuwa unapatikana katika nchi zote duniani.
Soma: Netflix sasa yapatikana dunia nzima.
Indonesia ndiyo nchi ya kwanza (ambamo Netflix ilishanza kutumika) kuzuia mtandao huu, ingawa bodi ya filamu Kenya ilitishia kuchukua hatua kama hii lakini haikufanikiwa kutokana na ata serikali ya nchi hiyo kutetea uwepo wa huduma hiyo. Wakisema ndio utandawazi na ukuaji wa biashara za kimataifa.
soma:Bodi ya filamu Kenya yasema Netflix lazima ifuate sheria.
Serikali ya Indonesia hata hivyo imesema kwamba huo ni uamuzi wa shirika na sio wa serikali na ndio maana makampuni mengine bado hayajaizuia Netflix. Afisa mmoja ameliambia gazeti la The wall Street Journal (ambalo ndilo liliripoti habari hii) kwamba Serikali yenyewe itafanya maamuzi mwezi mmoja baadaye na kuamua kama Netflix ifungiwe ama la.
No Comment! Be the first one.