Janga la Covid / Corona limewafanya wengi katika mataifa yaliyoathirika zaidi kutegemea huduma za kustream muziki na filamu kama njia ya kujipatia starehe.
Katika mataifa yaliyoathiriwa zaidi na Covid bado huduma nyingi za starehe kama vile muziki, baa na ata sinema bado hazifunguliwa. Hii inawafanya watu wengi kutegemea kujipa starehe kupitia filamu na muziki wakiwa majumbani.
Katika kipindi cha mwaka 2020 kufikia mwanzoni mwa mwaka 2021 kumekuwa na ukuaji mkubwa wa huduma za kutazama filamu na kusikiliza muziki kwa njia za mtandao, yaani kustream. Data zinaonesha huduma hizo zimepata watumiaji zaidi ya bilioni 1 katika kipindi hichi.
Soko la sinema lilipoteza mapato ya zaidi ya dola bilioni 30 kwa mwaka jana. Ingawa janga la Covid/Corona limechangia sana ila watafiti wengi wanasema ni jambo ambalo tayari lilikuwa linakuja, tayari watumiaji wengi walishaanza kutumia huduma za kustream zaidi.
Makampuni makubwa ya utayarishaji wa filamu kwa nchini Marekani (Studio za Hollywood) zimeshauliwa kuanza kujiandaa katika kutafuta namna ya kuendelea kutengeneza pesa kupitia huduma za kustream filamu mtandaoni.
Huduma zenye watumiaji wengi zaidi kufikia mwanzoni mwa mwaka huu
Kwenye filamu
1. Netflix
2. Amazon Prime
3. Apple TV
4. Hulu
Kwenye Muziki
1. Spotify
2. Apple Music
3. Amazon
Kwa Tanzania na Afrika mashariki kwenye eneo la muziki hali inaweza ikawa tofauti ila hatujafanikiwa kupata data rasmi. Tayari huku kuna huduma za kusikiliza muziki zenye watumiaji wengi na umaarufu mkubwa kabla ya ujio wa huduma ya Spotify na Apple Music. Huduma kama vile Boomplay na Mdundo Music ni huduma za muda sasa na tayari zina umaarufu mkubwa.
No Comment! Be the first one.