Katika 10 bora ya kampuni ambazo zinafanya vizuri kwenye mauzo ya jumla kwa miaka ya hivi karibu hakika huwezi kuwakosa Xiaomi ambao wamekuwa wakitoa rununu kadha wa kadha ikiwemo Xiaomi Redmi Note 10 Pro.
Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikifuatilia kwa karibu simu janja kutoka kwenye familia ya “Redmi Note” ambayo mpaka sasa wamefikia kwenye toleo la kumi ambalo sifa zake ni kama ifuatavyo:-
Kioo :
- Ukubwa: Urefu wa inchi 6.67
- Ubora: AMOLED (1080*2400px, 120Hz); ina ung’avu wa hali ya juu sana kufanya kinachoonekana kivutie
Memori :
- Diski uhifadhi: 64GB/128GB
- RAM: GB 6 na 8
Kamera :
- Kamera Kuu: MP 108, 8, 5 na 2+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 4K na 1080px
Kamera ya Mbele: MP 16+uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px na 720px

Betri/Chaji :
- Li-Ion 5020 mAh
- USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 33W (59% ndani ya dakika 30 tu)
Kipuri mama :
- Snapdragon 732G
Uzito :
- Gramu 193
Programu Endeshi
- MIUI 12, Android 11
Rangi/Bei :
- Kahawia, Shaba na Bluu
- Gharama yake inaanzia $299 (zaidi ya Tsh. 687,700) bei ya ughaibuni
Simu hii ina redio, sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, inatumia kadi mbili za simu, teknolojia ya kutumia alama ya kidole ipo kwa pembeni, mnara wa mawasiliano ni GSM / HSPA / LTE, Bluetooth 5.1, WiFi, NFC.
Haya wale wanaovutiwa na simu janja za Xiaomi nyingine ndio hiyo na sisi tumeshamaliza kazi yetu, uamuzi tunakuachia wewe msomaji wetu. Kaa nasi ili uwezi kuhabarika kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sayansi na teknolojia.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.