Miaka imesogea na teknolojia imekua pia; saa tulizokuwa tulizovaa miaka 10, 20, n.k iliyopita ni tofauti sana na hizi za leo ambazo zina mengi mbali ya kuonyesha muda (saa, dakika na sekunde).
Simu janja kwa kiasi kikubwa zimechukua nafasi ya watu kuwa na ulazima wa kuvaa saa mikononi mwao. Hata hivyo, kutokana na ukuaji wa teknolojia siku hizi kuna “Saa janja” ambazo zina uwezo wa kutufahamisha vitu vingi kuhusiana na miili yetu na hata nyingine kuwa mbadala wa simu ya kiganjani (kuwa na uwezo wa kupiga/kupokea simu, kutuma ujumbe, n.k).
Sasa ni wazi kuwa makampuni mengi tuu duniani yanatengenza hizi saa janja na mojawapo kati ya hayo ni Huawei ambao wapo njiani kuja na saa janja yenye uwezo wa kupima shinikizo la damu (blood pressure). Saa hii inaelezwa kuwa ya kitofauti na hizo ambazo Huawei imewahi kutoa huko nyuma kwa sababu:-
- muonekano wa kitofauti. Saa janja ambazo Huawei walishazitoa huko nyuma kioo chake ni cha duara ikiwa na vitufe viwili ama umbo la mstatili na kitufe kimoja cha kubonyeza kilichopo upande wa kulia wa saa husika.
Huawei Watch D: Saa janja ya Huawei ambayo ina uwezo wa kupima shinikizo la damu.
Waswahili husema “Mcheza kwao hutunzwa” na hapa nikimaanisha tayari Huwei imeshapata cheti cha kuitambua saa hiyo kama kifaa tiba kutoka mamlaka inayoshuguhlika masuala ya dawa nchini Uchina. Hata hivyo, inaweza kuchukua muda kwa saa hiyo kupata kibali kwenye nchi nyingine duniani.
Je, ewe msomaji wetu kitu unachokiovaa mkononi inakusaidia kufahamu afya ya mwili wako? Au wewe si mpenzi kabisa wa teknolojia ya aina hiyo? Tungependa kusikia kutoka kwako na kumbuka kutufuatilia kila siku kwani hakika utahabarika.
Vyanzo: GSMArena, Deccan Chronicle
No Comment! Be the first one.