Hyper wmeamua kuingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuendeleza kasi yao ya kutoa bidhaa ambazo zina kitu/vitu vya kipekee amabvyo vinazidi vingine; safari hii kimemeshi chenye nguvu sana.
Ni siku kadhaa tu Hyper walitambusha kumemeshi ambacho hakitumii waya na kina uwezo wa kuchaji AirPods lakini hiyo bado ikawa ni kitu cha kawaida sana na wakati huu wametoa kimemeshi ambacho unaweza kutembea nacho popote lakini kubwa zaidi kikiwa na jumla ya 130W.
Hyper Juice ndio jina la bidhaa yenyewe na imeelezwa kuwa inaweza kuchajiwa wakati ikiendelea kuchaji vitu vingine na mwisho wa siku vitu vyote vikajaa umeme.
Uwezo wake wa kuchaji vitu.
Kutokana na uwezo wa kifaa chenyewe (kuwa na zaidi ya 100W) kina uwezo wa kuchaji kipakatalishi ina ya Mac, iPad pamoja na iPhone vyote kwa wakati mmoja.
Muda unaotumika kuichaji.
usisahau kuwa Hyper Juice nayo ina betri amabalo linahitaji umeme ili kuweza kuchaji vifaa vingine. Mambo yapo hivi ukiwa na Hyper Juice yenye 60W itachukua zaidi ya saa moja na nusu kujaa lakini ile yenye 100W inachukua karibu saa nzima tu kupata umeme wake.
Ni kifaa ambacho kinavutia lakni mwisho wa siku inatubidi tuwe na $300|Tsh. 690,000 kuweza kununua kuanzia mwezi Novemba kitakapoingia sokoni.
Vyanzo: The Verge, Kick Starter