Simu zetu zina matumizi mengi zaidi lakini uchezaji wa magemu ni moja kati ya matumizi yanayoongoza zaidi kwa wengi katika simu zao. Na kupitia SmartBoy basi wengi watapewa sababu ya kufurahia zaidi magemu yao.
Kampuni moja nchini Marekani imeamua kuleta wazo lililokuwa limeletwa kiutani siku ya wajinga duniani mwaka huu, mwezi wa nne, kuwa halisi. Wazo hilo ni kuwa na kifaa kidogo (gadget) kitakachounganishwa na simu janja kuweza kurahisisha zaidi uchezaji wa magemu – Gamepad. Kifaa hicho kitafahamika kwa jina la SmartBoy
Tayari kampuni hiyo ipo katika hatua za utengenezaji wa gamepad hiyo kwa ajili ya simu ya iPhone 6 Plus. Wamesema tayari wanaangalia kuja kuleta uwezo wa kifaa hicho kwenye simu za Android na Windows pia.
Hyperkin, kampuni inayotengeneza kifaa hicho haijatoa bado tarehe rasmi ya watu kutegemea kifaa hicho kuingia sokoni ila tayari wapo kazini ili kuweza kukileta.
Je uchezaji magemu kwenye simu ni moja kati ya matumizi yako makubwa ya simu? Je unaweza kununua SmartBoy kikianza kupatikana?
No Comment! Be the first one.