Apple imeshazindua iPhone 15 na imekuakua simu ambayo ina vipengele vingi vipya licha ya simu pia iCloud na yenyewe imepata ujazo uhifadhi mpya.
Ni wazi kwamba iCloud ni ya bure lakini unapewa ujazo uhifadhi mdogo na kama ukitaka ujazo uhifadhi wa juu Zaidi basi hauna budi kuulipia (kuna vifurushi kabisa).
Apple wametangaza kabisa kwamba kuna vifurushi viwili vipya ambavyo ni 6TB na 12TB, ukifikiria huu ni uwezo mkubwa sana maana ujazo uhifadhi huo ni mwingi sana.
Kwa wale ambao hawajui ni kwamba iCloud ni huduma ya Apple ambayo inahusisha kuhifadhi picha, mafaili, notisi, password na taarifa zingine za muhimu katika mtandao (Mtandao wa Apple).
Kingine ni kwamba iCloud pia inasaidia sana kama kifaa chako hakina ujazo uhifadhi mkubwa, maana unaweza kuhifadhi kwenye mtandao na kufuta kwenye simu.
iCloud inaweza kutumika na watu hata watano ambao wanaweza wakawa wana’share library ya picha kwa pamoja kutumia mtandao huo.
Kwa sasa kwa kawaida ni kwamba iCloud ambayo sio ya kulipia na kila mtu anaweza akawa nayo inakua inatoa GB5 za bure tuu.
Hii inaonekana wazi kwamba huu ni ujazo uhifadhi mdogo sana maana siku hizi teknolojia inakua mafaili yanakua makubwa Zaidi, picha zinakua nzuri Zaidi na hiyo inamaanisha kuwa zitakau na ukubwa Zaidi.
Hii ndio maana vinakuja vifurushi kama hivi kutoka kwao iCloud, na vifurushi hivyo vitaanza kupatikaana mwezi huu tarehe 18 na havitegemewi kuwa na bei ndogo.
Nipenda kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment je hii unalichukuliaje? Je uko radhi kununua ujazo uhifadhi wa mtandaoni?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.