iCloud.Com yapata muaonekana mpya katika kompyuta –pengine hili ni kuendana na hali halisi – na hii ni baada ya kupitia majaribio mengi ya toleo hili.
Muonekano mzima wa iCloud umebadilika tofauti kabisa na mwanzo, na vipengele vingi ambavyo vipo vinakufanya uhisi kama bado unatumia kifaa chako kile kile (iPhone au iPad).
Kwa sasa ukifungua tuu mtandao huo kupitia katika kompyuta utakutana na App za Apple kama Photos, Mail, iCloud Drive, Calendar, na Notes.
Ili kupata App zingine ambazo kwa kawaida huwa zinapatikana katika mtandao huo haina budi kuingia katika menu –ina alama ya nukta nukta nyingi – ili kupata app kama vile Find My, Pages, Numbers, Keynote na zingine nyingi ambazo hazipo katika uso wa mbele kabisa.
Kingine kizuri ni kwamba kwa mtumiaji anaweza akamua kupangilia App hizo na kuwa katika mpangilio ambao anautaka yeye n.k
iCloud ni moja kati ya mitaandao maarufu sana ambayo inatoa huduma ya ujazo uhifadhi wa mtandao licha ya kuwa moja kati ya njia kuu ya kufidhi baadhi ya vitu kwa njia ya mtandao kwa vifaa vya Apple.
Sio mara kwa mara huwa tunapata maboresho au muenekano mpya kwa mtandao mzima na ndio maana hata mitandao huo haibadilishi mounekano mara kwa mara lakini kwa iCloud ili kuendana na uhalisia katika vifaa vya Apple ilibidi tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je umeshaanza kutumia muonekano huu mpya? Niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.