Simu janja za ule mfumo wa kujikunja (fold) ziliingia katika soko na mapokezi yake sio mabaya hii inaonyesha dhahiri kwamba kwa kipindi kijacho soko lake litapanuka zaidi.
Mwaka 2022 ndio mapinduzi makubwa yalifanyika kuhisiana na simu hizi –fold– na kingine ni kwamba mpaka sasa bado kampuni ya Samsung imeshika usukani katika aina ya simu hizi huko sokoni.
Hii inasemekana kutoka na repoti ambayo imetolewa na IDC ambao wao kwa utaalam wao wameona dhahiti kwamba simu za aina hii katika soko zitaongezeka maradufu kabisa.
Ni wazi kwamba katika soko kwa sasa simu janja za kawaida ndio zimeshikilia soko kwa kiasi kikubwa sana lakini hii haimaanishi kwamba simu janja za aina nyingine haziwezi fanya hvyo pia.
Ripoti hiyo kutoka IDC ni ya utabiri tuu, na utabiri huo unaonyesha dhahiri kwamba mpaka kufikia mwaka 2027 vifaa milioni 48.1 vitakua vimefikia mauzo kwa mwaka
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Simu Janja Za Kujikunja >>HAPA<<
Kwa kawaida simu za aina hii huwa zinauzwa bei kubwa na hiyo ni ukilinganisha na simu janja za kawaida na hii yote ni kutokana na kwamba utengenezajwi wake ni tofuuti kabisa na simu zingine.
Watengenezaji wengi wa simu janja za kujikunja (fold) kwa sasa wanakua na wakati mgumu sana katika kuhakikisha kuwa wanatengeneza simu za aina hii na kisha wanaziwekea bei ndogo zinapoingia sokoni.
IDC ni Shirika la Kimataifa la Takwimu
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani hali itakwenda kama utabiri unavyosema? Je kuna kipindi itafikia simu za aina hii kuzipiku hata simu janja za kawaida katika soko? naindikie hapo chini katika eneo la comment, ningependa kusikia kutoka kwako.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.