Android O ni jina ambalo imepewa programu endeshaji ijayo kutoka Android ambayo inamilikiwa na Google. Kwa maana nyingine hii inaweza ikajulikana kama Android 8.0
Kwa sababu ya sasa inaitwa Android 7.0 au Nougat. Android O kwa haraka haraka ni kwamba itakua na maboresho ya aina yake ukilinganisha na matoleo ya nyuma.
Kumbuka Android ndio programu endeshaji inayoongoza kutumia zaidi duniani katika simu janja na vifaa vingine.
Inavyosemekana ni kwamba programu endeshaji hii itatolewa rasmi agosti 21, 2017 na hii ni siku chache tuu kutoka sasa.
SIFA ZAKE KWA UCHACHE
- Maboresho katika eneo la Notification
- Maboresho katika Background Apps, kwa kudhibiti matumizi
- Maboresho katika ku’copy na ku’paste
- Maboresho katika soko la Google Play ambapo utaweza kuweka ‘pause’ update yeyote ile ili kufanya data isitafunwe (kutumika katika zoezi hilo)
Ukiachana na hayo kutakua na maboresho mengine kadha wa kadha ambayo tutayaweka wazi programu endeshaji hii ikitoka rasmi