Ni wazi kwa sasa soko la tabiti sio kubwa kama ilivyokua hapo awali, Tableti kuna muda zililiteka sana soko maana zilikua zipo nyingi sana.
Ni makampuni mengi yameeachana kabisa na uzalishaji wa tabiti… zilivyoingia tuu zilikua ziko katika ya simu janja na kompyuta mpakato. Wao Samsung kwa sasa wana mpango wa kuja na tabiti mpya inayojulikana kama Galaxy Tab S9 Ultra.
Kwa upande wa Samsung wao ndio kwanza wanatangaza ujio mpya wa tabiti inayojulikana kama Samsung Galaxy Tab S9 Ultra.
Hii inaonyesha dhahiri kwamba licha ya vifaa vya aina hii kushuka kimauzo katika soko bado kuna makampuni kama vile Samsung ambayo bado yanahakikisha wateja wake wanapata bidhaa za aina hii.
Ikumbukwe katika teknolojia ya simu Samsung ndio amabe anaongoza kuuza simu janja zenye mfumo endeshaji wa Android katika soko.
Ukija katika soko la tabiti huku Apple ndiye alieshikilia usukani, na hili limefanikiwa kudumu kwa kipindi cha muda mrefu sana… pengine Samsung anajifua kuja kumpita Apple?
Samsung Galaxy Tab S9 Ultra.
Ukiachana na wembamba wake wa hali ya juu ni bado itakua na sifa za aina yake ambazo zinatofautisha kabisa toleo hili na tabiti zingine za nyuma kutoka katika kampuni ya Samsung.
Tabiti hii ambayo inakuja kutokea Samsung itakua inakuja na baadhi ya sifa zinazopatikana katika vifaa vya Galaxy S23, Galaxy S23+ na hata Galaxy S23 Ultra.
Yaani kwa maana kwamba itakua na Snapdragon kizazi cha 8 kwaajili ya Prosesa za Galaxy RAM 16GB LPDDR5X ambayo kwa itaongeza ufanisi kwa kiasi kikubwa sana.
Uwezo wa betri pia utakua umeongezwa mpaka kufikia 11,200mAh na uwezo wa kuchajiwa kwa haraka (fast charging) ambao ni 45W.
Itakua na uwezo wa kuzuia uchafu/fumbi kuingia ndani na hata maji na ikumbukwe tuu tabiti hii kutoka Samsung ndio ambayo itakua tabiti yenye hadhi ya juu sana kutoka kwao labda mpaka kampuni itoe toleo lingine.
Tabiti hii inategemewa kuingia sokono katika nusu ya pili ya mwaka 2023 na kingine kikubwa ni kwamba sifa zake zote zitaongelewa siku ya uzinduzi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je wewe ni mpenzi wa tabiti? Niambie kwa namna tabiti hii inavyopambwa je unaweza kuitumia? Vipi kuhusu iPad je wajiandae kwa ushindani zaidi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.