Xiaomi wanafahamika kwa kutoa simu janja mbalimbali zikiwemo zile zenye uwezo zaidi zikilenga wapenzi wa kucheza magemu kupitia simu za viganjani. Black Shark 4 ni mojawapo ya simu janja zenye uwezo mkubwa wa kuhimili magemu.
Mimi ni mmoja kati ya watu wengi ambao tunapenda kucheza magemu kupitia simu ya kiganjani na kwa maana hiyo basi rununu ikiwa na uwezo mkubwa hasa kwenye RAM na kipuri mama lakini bila kusahau urefu wa kioo inanifanya nisikie burudani kabisa ninapoburudika kwa kucheza magemu.
Black Shark 4 inaelezwa kuwa ni ya pili kutoka Xiaomi kwa rununu zilizo kwenye kundi ya wale wanaopenda kucheza magemu kupitia rununu. Sifa zake ni kama ifuatavyo:-
Kioo :
- Ukubwa: Urefu wa inchi 6.67
- Ubora: Super AMOLED (1080*2400px, 144Hz); ina ung’avu wa hali ya juu sana kufanya kinachoonekana kivutie
Memori :
- Diski uhifadhi: 128GB/256GB
- RAM: GB 6/8/12
Kamera :
- Kamera Kuu: MP 48, 8 na 5+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 4K na 1080px
- Kamera ya Mbele: MP 20+uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
Black Shark 4: Muonekano wa nyuma na mpangilio wa kamera. Upnde wa mbele/nyuma unalindwa na Gorilla Glass.
Betri/Chaji :
- Li-Ion 4500 mAh
- USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 120W (100% ndani ya dakika 17 tu)
Kipuri mama :
- Snapdragon 870G 5G
Uzito :
- Gramu 210
Programu Endeshi
- Joy UI 12.5, Android 11
Rangi/Bei :
- Nyeusi, Fedha na Bluu
- GB 6/128-$439 (zaidi ya Tsh. 1,009,700), GB 8/128-$489 (zaidi ya Tsh. 1,124,700), GB 12/128-$699 (zaidi ya Tsh. 1,607,700) na GB 12/256-$599 (zaidi ya Tsh. 1,377,700) bei ya ughaibuni
Ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, inatumia kadi mbili za simu, teknolojia ya kutumia alama ya kidole ipo kwa pembeni, mnara wa mawasiliano ni GSM / CDMA / HSPA / EVDO / LTE / 5G, Bluetooth 5.2, WiFi, NFC.
Haya sasa wale wapenzi wa kucheza magemu kwa kutumia simu ningependa kusikia maoni yenu na simu hii ina toleo la Pro ambapo zinatofautiana kidogo tuu.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
One Comment