Kwa mwaka huu moja ya vitu ambavyo watu wengi walikuwa wanasubiri kuweza kuvijua undani wake kuoka Huawei ni tabiti-MatePad Pro 2021 5G amabayo mengi yslielezwa lakini hatime sasa sifa zake zote zimefahamika.
Muda mrefu tuu zilikuwepo taarifa kuwa baadhi ya bidhaa za Huawei zitakazotoka zitakuwa na upekee wa aina yake na mojawapo ya vitu hivyo ni MatePad 5G ya mwaka 2021. Katika vitu ambavyo Huawei imejitofautisha na washindqani wake wengine ni kuweka prograqmu endeshi (HarmonyOS) waliyoitengeneza wao wenyewe kwenye tabiti yao hii mpya.
Vitu vingine ambavyo binafsi vimenivutia ni teknolojia ya 5G, spika nane, kutoa toleo mbili (inayotumia WiFi/kadi ya simu) lakini bila kusahau uwezo mkubwa betri. Kufahamu mengi zaidi kuhusu MatePad Pro 5G soma makala hii hadi mwisho.
- Ukubwa: Urefu wa inchi 12.6
- Ubora: OLED (2560*1600px); ina ung’avu wa hali ya juu sana kufanya kinachoonekana kivutie
- Diski uhifadhi: 128GB/256GB+uwezo wa kuongeza memori ya ziada mpaka GB 256
- RAM: GB 4/8
- Kamera Kuu: MP 13, 8 na TOF 3D+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 4K na 1080px
Kamera ya Mbele: MP 8+uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
- Li-Ion 10050 mAh
- USB-C 3.1, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 40W, reverse charging 5W, kuchaji bila kutumia waya 27W, reverse wireless charging 10W
- Kirin 9000E 5G (WiFi)
- Kirin 9000 5G
- Gramu 609
Programu Endeshi
- HarmonyOS 2.0
- Fedha, Kahawia na Kijani
Gharama yake inaanzia $943 (zaidi ya Tsh. 2,168,900) bei ya ughaibuni
Bidhaa hii tayari ipo sokoni tangu mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu na hiyo ndio tabiti ambayo Huawei wanayojivunia nayo sokoni.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.