Ruta ni kifaa muhimu sana hasa katika kizazi hiki cha simu janja, tableti n.k, ni kifaa ambacho kinauwezo wa kukupatia huduma ya intaneti kwa mfumo wa WiFi, kila mahali ambapo unapata mawimbi ya WiFi basi eneo hilo linatumia kifaa kinachoitwa ruta.
Pamoja na faida hizi za ruta, kuhakikisha kuwa ruta yako ipo katika ubora wake na kuiweka tayari kwa matumizi kunaitaji ujuzi flani. Kuliona hilo kampuni ya Google imeamua kutengeneza ruta ambayo haita hitaji ujuzi wa kiufundi kuitumia.
OnHub ni ruta mpya iliyotengenezwa na kampuni ya Google, ruta hii ni nyepesi kuitumia haihitaji ujuzi wa kiufundi kutatua matatizo yake. OnHub imebuniwa katika umbo ambalo linamvuto na hivyo haitaharibu mandhari ya mahali itawekwa, pamoja na hayo ruta hii imepewa uwezo wa kuwasha na kuzima vifaa mbali mbali ndani ya nyumba (Home automation system)
Tofauti na ruta nying OnHub yenyewe inaweza kusetiwa kwa kutumia vitumizi (app) vya android ama iOS, hii inamana kuwa ukiwa na simu yako yenye kitumizi hicho unaweza kuipangilia (setting) ya ruta yako bila shida yeyote. Utaweza kuona vifaa vyote vilivyo unganishwa katika ruta kwa kutumia simu yako janja na pia utakuwa na uwezo wa kuchagua ni vifaa gani vipewe kipaumbele katika kutumia mtandao.
OnHub ina antena 13 ambapo 6 kati ya hizo ni kwaajiri ya masafa ya 2.4GHz na 6 nyingine ni 5GHz na moja ni kwaajiri ya kuangalia msongamano. OnHub itaweza kutoa mtandao wenye kasi ya 1900Mbps pia itakuwa na nafasi ya GB 4 kwa ajili ya kuhifadhi mafaili yako.
No Comment! Be the first one.