Sheria ya makossa ya kimtandao inaangazia sanasana katika makossa na adhabu ambazo zinatokana na matumizi ya (kifaa cha) kompyuta na TEHAMA.
Sheria hii imetokea baada ya ukuaji wa matumizi ya TEHAMA kuongeza kwa kasi sana nchini Tanzania. Ikumbukwe kwamba makosa yanayofanywa katika mtandoa sharia zake ni tofauti kabisa na sheria za makosa mengine.
Kuna mambo mengi tuu ambayo yanaonyesha utofauti kati ya makosa tuliyoyazoea na haya ya mtandaoni kwa mfano sio lazima kitu kilichoibwa kihamishike. Na lingine la muhimu ni kwamba sio lazima makosa ya kimtandao yafanyike ndani ya mipaka ya nchi husika.
Sheria ya makosa ya kimtandao ilipitisha na Bunge tarehe Mosi Aprili 2015 na kuidhiniswa na rais wa Tanzaia Aprili, 25 2015. Ili mtu aadhibiwe kisheria ni lazima kosa lianishwe kwenye kanuni za adhabu au litambulike kisheria.
MASUALA MUHIMU KWENYE SHERIA HII (MAKOSA).
- Utoaji na ukusanyaji wa maudhui katika mtandao,
- Picha za ngono (wakubwa/watoto),
- Utoaji wa taarifa za uongo,
- Ujumbe unaotumwa bila ridhaa,
- Matusi ya kibaguzi,
- Kuzuia upelelezi,
- Unyanyasaji kupitia mtandao kula njjama ya kutenda kosa,
- Ukiukwaji wa haki bunifu,
- Ulinzi wa miundombinu muhimu ya TEHAMA,
- Makosa dhidi ya ubinadamu.