Usiku wa kuamkia jumapili hii mji wa Orlando Florida ulikumbwa na huzuni baada ya mwanaume mmoja kuvamia kablu moja ya watu wenye mahusiano ya jinsia moja na kufyatua risasi, inakadiriwa mpaka sasa takribani watu 49 wamepoteza maisha yao katika tukio hili.
Omar Mateen mwanaume anayeshukiwa kufanya matukio hayo na ambaye aliuwa na maafisa usalama katika tukio hilo aliingia katika klabu hiyo mida ya saa nane usiku akiwa na bastola pamoja na bunduki aina ya .223 AR Rifle pia alikuwa na kiasi kikubwa cha risasi kwaajiri ya kutekeleza tukio hilo ambalo alilipanga kwa muda mrefu.
>AR rifle na matukio ya kigaidi Marekani
Bunduki aina ya AR Rifle imekuwa ni chaguo la wahalifu wengi ambao wanalenga kuua watu wengi ndani ya muda mfupi, yafuatayo ni baadhi ya matukio ambayo silaha kama hii ilitumika.
- Disemba 2015
Silaha hii ilitumiaka katika tukio la kigaidi lililofanyika San Bernardino Disemba mwaka jana ambapo watu 14 waliuwawa, tukio hili liliwahusisha mtu na mke wake ambao waliwashambulia wafanyakazi waliokuwa katika sherehe ya mwisho wa mwaka.
- 2012
Silaha hii ilitumiwa mwaka 2012 katika matukio mawili, la kwanza ni pale ambapo mshambuliaji alipofyatua risasi kwa watu ambao walikuwa katika ukumbi wa sinema huko Aurora Colorado. Katika tukio jingine huko mjini Newton Connecticut mshambuliaji alifyatua risasi katika shule ya watoto na kuwaua watu 26 wengi wao wakiwa watoto.
>Mambo matano muhimu kuyajua kuhusu silaha hii iliyotumika katika mauaji haya makubwa zaidi katika hisoria ya marekani.
- Kwa mara ya kwanza bunduki za aina hii zilitengenezwa mwaka 1959 kwa ajiri ya majeshi ya Marekani.
- Aina hii ya bunduki ilifanyiwa mabadiliko yaliyopelekea kutengenezwa bunduki maarufu ya M16.
- Kwa miaka hii bunduki hizi zinatengenezwa na makampuni mengi kwaajiri ya nchi mbalimbali kwa matumizi ya kijeshi na pia kiraia.
- Silaha za aina hii zinapendwa zaidi kwa kuwa ni rahisi kubebeka na pia zina uwezo mkubwa wa ufanisi.
- Inaweza kubeba magazini za ukubwa tofauti.
Nini mtazamo wako juu ya sheria lele mama za umiliki na udhibiti wa silaha nchini Marekani?
Soma Pia – Marekani Watengeneza Risasi Yenye Uwezo wa Kukata Kona
Habari hii imeandikwa kwa msaada wa vyombo mbali mbali vya habari ambavyo viliripoti tukio hili kama vile ABC na vinginevyo