Starlink ni mtandao wa intaneti/internet unaosimamiwa na kampuni ya SpaceX ambao unatumia teknolojia ya satelaiti ili kupeleka intaneti kwa watu popote duniani, StarLink Ilizinduliwa rasmi mnamo mwaka 2018 na mmliki wake si mwingine bali ni Elon Musk ambaye anamiliki kampuni ya SpaceX, Tesla na pia ni mmliki wa mtandao wa Twitter.
StarLink inalenga kutoa huduma ya internet yenye kasi hasa kwa maeneo yasiyo na huduma ya mtandao wa simu au mtandao wa nyaya. Mtandao wa Starlink unatumia maelfu ya satelaiti zilizowekwa katika obiti ya anga ya juu kuzunguka dunia.
Kwa kufanya hivyo, inawezesha watu kuwa na ufikiaji wa intaneti katika maeneo yasiyofikiwa kwa urahisi na miundombinu ya kawaida ya mtandao wa simu au nyaya. Kulingana na SpaceX, teknolojia hii inawezesha kutoa intaneti yenye kasi kuanzia 50Mbps hadi 300Mbps.
Moja ya faida kubwa ya Starlink ni kwamba inatoa ufikiaji wa mtandao wa intaneti kwa maeneo ambayo yamekuwa hayafikiwi na huduma ya mtandao wa simu au nyaya. Hii ni pamoja na maeneo ya vijijini, maeneo ya mbali, na hata maeneo ya jangwa ambapo miundombinu ya mtandao haijafikiwa.
Hii inaweza kuwa muhimu kwa watu wanaofanya kazi kutoka nyumbani, wapenzi wa burudani, wapiga picha na watumiaji wengine wa mtandao. Lakini kama ilivyo na teknolojia yoyote, Starlink pia ina changamoto zake. Moja ya changamoto kubwa ni gharama ya huduma hii, Wateja wa Starlink wanahitaji kulipa gharama ya kuanzisha huduma ikiwemo kununua vifaa pamoja na ada ya kila mwezi ili kuweza kuendelea kutumia huduma hii. Bei hii ni kubwa ikilinganishwa na huduma za mtandao wa simu au nyaya. Ikiwa gharama ya kununua vifaa inakadiriwa kuwa si chini ya Tsh 1,400,000 na gharama za kulipia kwa mwezi inaanzia Tsh 257,290 nakuendelea.
Pia, teknolojia ya satelaiti ina changamoto za kiufundi satelaiti inahitaji angalau 40ms ya ping (uwezo wa mawasiliano ) kati ya ardhi na satelaiti, hivyo Starlink inapunguza ping kwa kupunguza urefu wa obiti ya satelaiti (kwa 550km kutoka kawaida ya 1000km), hii inamaanisha kuwa satelaiti hulazimika kuzunguka dunia kila dakika 90 kwa hiyo hutoa huduma ya intaneti isiyo thabiti kwa sekunde chache kila baada ya dakika 90. Kwa ujumla, Starlink ni teknolojia ya kuvutia sana ambayo ina uwezo wa kutoa intaneti kwa maeneo yasiyofikiwa na miundombinu ya mtandao wa simu.
Intaneti ya StarLink imekuja kuleta mapinduzi kwenye namna ya utoaji wa huduma wa internet ikiwa inaweza kutumika sehemu zot hata zile ambazo hazijafikiwa na miundombini ya simu au nyaya. Tanzania hatuna hii huduma kwa sasa.
Unaweza pia kusoma makala zetu zingine hapa.
No Comment! Be the first one.