Apple ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika swala zima la teknolojia na kila mwaka huwa watu wanasubiria kwa shauku kuona ni nini wanatoa katika mwaka husika.
Apple ina bidhaa na huduma nyingi sana ambazo huwa zinawaingizia hela nyingi na kuifanya kuwa moja kati ya makampuni ye teknolojia ambayo ni tajiri sana.
Kumbuka iPhone ndio inaonekana kama ni bidhaa kubwa sana kwa kampuni lakini kuna bidhaa na huduma zingine nyingi tuu ambazo nazo ni muhimu kwa kampuni.
Kwa mwaka 2024 niasemekana watakuja na bidhaa hizi.
Inasemekana kampuni imeweka mpango mkakati kwa vifaa vyote ambavyo vinavalika –Saa, visionPro na Airpods) vitapata masasisho (Updates) makaubwa.
Ni wazi kwamba VisionPro itakua ndio inaingia katika soko lakini kifaa kama cha Airpod kitatoka kingine cha gharama ndogo zaidi kulinganisha na hiki ambacho kipo katika soko.
Kifaa hiki pia kitakua kinatumia chaja ile ya aina ya USB type-C na itakua na uwezo wa kuachana na sauti za mazingira ya nje (voice cancelation)
Vile vile katika upande wa saa kampuni ina mpango wa kubadili muonekano wa saa janja moja licha na hivyo bado wana mpango wa kuongeza vipengele vingi vya kiafya katika saa hiyo.
Mwaka 2024 apple inajikita zaidi mpaka kwa vifaa vingine ili kuhakikisha vifaa hivyo vinaingiza pesa nyingi kwa kampuni.
Kumbuka kwa sasa iPhone inaleta asilimia 50 ya mapato kwa kampuni, huku bidhaa na huduma zingine zikijikongoja tuu.
Baki nasi ili kuzidi kupata habari za kina juu ya vifaa vya Apple na huduma zake pale tuu zinapotoka lakini kubwa ambalo linasubiriwa kwa mwaka 2024 ni uzinduzi wa VisionPro
Kingine ni kwamba hii haimaanishi kwamba kwa mwaka 2024 hakutokua na toleo lingine la iPhone, hili liko pale pale na inasemekana toleo la iPhone 16 lenye kioo kikubwa zaidi linaweza likatoka.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je kwa upande wako ni kifaa gani ambacho unakisubiria kwa hamu zaidi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.