India ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo ambayo yatairuhusu kununua ndege zisizo na rubani kutoka kampuni ya kimarekani, makubaliano haya yataipatia ndege zisizo na rubani aina ya Predator XP 4o kwa kuanzia.
India inataka kuzitumia ndege hizi kuongeza ushawishi wake kijeshi katika nchi za Asia na pia kwajiri ya kuilinda mipaka yake na china pamoja na Pakistani, nchi hiyo ambayo tayari ilikwisha nunua ndege kama hizi kutoka katika kampuni ya Israel hivi karibuni inategemea kwamba baada ya dili hili itaweza kununua tena ndege nyingine ambazo zitakuwa zinauwezo wa kubeba siraha.
Predator XP ni ndege zisizokuwa na rubani ambazo kazi yake kubwa hasa nikufanya ushushu na zimekuwa zikitumiwa kwa kipindi sasa na nchi ya marekani kwaajiri ya kukusanya taarifa za kijasusi.
India imekuwa katika misuguano na majirani zake wakubwa Pakistani na China hasa kuhusu mipaka yake, Pakistani juu ya jimbo la Kashmiri ambalo limekuwa likigombewa na nchi hizimbili kwa miaka sasa na kwa upande Wa china ni msuguano unakuja baada ya China kuongeza shughuli zake katika bahari ya hindi hivyo ni wazi kwamba India inataka nayo kulinda mipaka yake zaidi na kukusanya taarifa za kijasusi.
Zaidi ya ndege zinazojiendesha zenyewe kwa ajiri ya kukusanya taarifa na kulinda mipaka India imeweka wazi mipango yake ya kununua ndege nyingine zinazojiendesha zenyewe lakini ambazo zinabeba mabomu kama zile ambazo zinatumiwa na majeshi ya marekani katika operesheni zake huko Iraki pamoja na Afghanistan.
Ingawa ili dili hizi zote zikamilike inabidi zijadiliwe na bunge la seneti la huko Marekani lakini wataalamu wa mambo wanasema kwamba kwa kuwa Marekani inaichukulia India kama ni mshirika katika eneo la Asia mashariki basi ni dhahiri kwamba India itapata ndege hizi.
Lakini manunuzi haya ya ndege za kivita ambayo kimsingi yanaliongezea jeshi la India uwezo kijeshi sio habari nzuri kwa Pakistani pamoja na China ambazo zinaona India inafanya manunuzi haya ya siraha kuonesha kwamba ipo tayari kwa lolote.
Chanzo: REUTERS