India ni moja kati ya nchi ambazo zinathamini sana ulinzi na usalama haswa ule wa taarifa (data) za watu wake na sasa wanaijia nchi ya china juu.
Japokua wako mstari wa mbele na china lakini ni wazi kwamba wanaziangalia nchi nyingine kubwa kubwa katika bara hilo la asia, App watakazokua na mashaka nazo jambo hili litazikumba.
Kwa taarifa ambazo mpaka sasa zipo ni kwamba mpaka sasa India ishaanza kuchukua hatua kwa App 240 za kubeti na zile za kutoa mikopo ambazo zinahusika moja kwa moja na nchi ya china.
Kikubwa kinachoogopwa hapa ni kwamba kuna hofu kubwa kwamba kampuni hizo kutoka china zinaleta mashaka makubwa kwa watu maana inasemekana kuwa App hizo zinakusanya taarifa za wateja wake.
Licha ya kuzikushanya tuu taarifa hizo, mwisho wa siku zinaenda kutumiwa na serikali ya china hali ambayo inawafanya wengi kujiuliza maswali mengi.
Hii si mara ya kwanza kwa kampuni kutoka china, au serikali ya china kwa ujumla kupata shutumu ya kuwa kwa kutumia App n.k huwa wanakusanya taarifa za watu.
Ukaichana na jambo hili bado kuna shida baina ya nchi hizi mbili yaani china na india na utata huo uko mpakani mwa nchi hizi mbili.
Ukiachana na App hizo ambazo tayari zimeshaanza kufanyiwa kazi na serikali ya India bado nchi inasema kuwa haijaishia hapo na App nyingi zaidi zitaweza kupigwa marufuku.
Ni wazi kwamba makampuni mengi kutoka china yamekua yakipata hii shutuma, kampuni kama Huawei ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa sana katika soko la simu janja yalipata shutuma hii na kufungiwa katika mataifa mbalimbali
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani ni sahihi kwa nchi kufungia App kisa inahisi inadukua taarifa za wateja wake?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.