Baada ya tovuti mbalimbali maarufu kama GSMArena, XDA Developers kuandika makala ya uzinduzi wa Infinix ZERO X na kutupia Picha…
… Inayoashiria ni kamera za Infinix ZERO X nyuma ikiwa na kamera 3 na kwa inavyosemekana kamera kuu ni MP108 OIS Ultra Resolution.Â

Bado haijatosha wataalamu wa maswala ya nyota na mwezi ‘Royal Observatory Greenwich’ ambao ni washirika na Kampuni ya simu Infinix katika kuileta Infinix ZERO X nao wameonekana kusifia zaidi teknolojia ya 60X periscope zoom lens ya Infinix ZERO X.
Wataalamu hao wa nyota (Astronomers) wanadai baada ya tafiti waliyofanya wamebaini kuwa 60X periscope Zoom Lens ya Infinix ZERO X inauwezo wa kupiga picha za Anga kama mwezi n.kÂ
Sifa hizo zimeonekana kuwachanganya wadau wa simu za Infinix katika nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambapo simu hii bado kuzinduliwa.
Shauku ni kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii wengi wakihoji je simu hii itatua lini Bongo na je itakuwa na sifa sawa na hii inayoonekana kusifiwa zaidi mitandaoni?

Kampuni ya simu Infinix bado haijaongea rasmi kuhusu hili isipokuwa dalili ya mvua ni mawingu kwani kupitia @infinixmobiletz kunaashiria ujio wa kitu kipya.
Hebu tukae mkao wa kula huku tukisubiria tamko kuu kutoka kwa kampuni ya Infinix, vile vile usisahu kuchungulia katika mitandao yao ya kijamii maana siku yeyote unaweza ukashangaa wanatoa mzigo.
Niambie hii Kutoka kampuni ya simu ya Infinix Umeipokeaje? je ulishawahi fikiria kama simu inaweza kupiga picha za anga?
Vile vile hivi umesikia fununu zingine zozote kuhusu simu hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.