Katika maisha ya kidijitali kuna vitu vingi tuu ambavyo vinaweza kuwa mkombozi kwa mtu mmoja mmoja au kundi la watu kwa kuwawezesha kupata kipato na moja ya njia hizo ni kwa kutumia matamasha ya Facebook.
Kutokana na mbinu za kujikinga na virusi vya Corona duniani kote tumekuwa tukishauriwa kutumia teknolojia kutimiza majukumu yetu tukiwa majumbani lakini kazi zetu za ujenzi wa taifa na kujiingizia kipato zikiendelea kama kawaida.
Vilevile, tufahamu kuhusu kwa kile nilichokiita “Matamasha ya Facebook” kwa mujibu wa tafsiri au Kiingereza ni Facebook Events ambapo kwa yeyote yule mwenye ukurasa wake Facebook anaweza akaandaa tamasha ma kulintangaza kwa watu wanaomfuatilia. Mathalani ambavyo TeknoKona tumelivyoweza kurusha mkutano wa wataalamu wa TEHAMA mwaka 2018 mubashara kupitia ukurasa wetu wa Facebook.
LakiniFacebook wameamua kuwezesha waandaaji wa matamasha haya ya Facebook yaweze kuingiza kipato na hii ikiwa ni hatua moja zaidi mbali tuu na kuwafahamisha watu kuhusu tukio husika.
Kivipi? Unapotengeza tamasha la Facebook unaweza ukalitangaza tamasha lako (ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi), kuweka kiwango cha watu kulipia ili kuweza kuliona kitu ambacho kitawezesha mwandaaji kuweza kuingiza pesa.
Mfano wa tamsha la Facebook ambalo mtu anaweza akalipia kuweza kushiriki.
Katika kipindi hiki ambapo wananchi kwenye nchi nyingi wapo ndani tuu hii inaweza iklawa ni njia mojawapo ya wao kujiingizia kipato wakiweza kuwafikia watu wao na kufurahi pamoja. TeknoKona tunasema ahsante teknolojia 😆 😆 .
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|