Kipengele cha “Stories” kwemye Instagram kimekuwepo kwa miaka sasa na kimekuwa kikifanyiwa maboresho ambayo huwa yanapokelewa katika mtazamo chanya na hasi.
Facebook ambayo ndio inamiliki Messenger, WhatsApp, Instagram imekuwa ikileta maboresho kwenye programu tumishi ambazo inamiliki. Wataalamu wa uandishi wa programu wapo kazini kuleta maboresho kwenye kipengele cha “Stories” ndani ya Instagram hivyo kukifanya kivutie kwa namna yake.
Swali dgogo tuu; Instagram stories ni nini?
Hiki ni kipengele ambacho kinapatikana kwenye Instagram, Facebook ambacho mtu anaweka chapisho lake (inaweza kuwa picha, picha mnato au ujumbe wa maandishi) na mara baada ya mhusika kupandisha hewani kile ambacho anataka wengine wakione kinakuwa kwenye uso wa mbele juu kabisa hivyo kuonekana kwa urahisi.
Watumiaji wa Instagram mtakubaliana na mimi kuwa tunaperuzi machapisho ya watu kwenye Instagram Stories lakini hatuna uwezo wa kuonyesha kuwa tumevutia na chapisho fulani, si ndio? Hilo sasa huenda likabadika kwani kuna maboresho yanapikwa ambayo yatamwezesha mtumiaji wa Instagram kuonyesha hisia zakekuhusu chapisho fulani kwenye “Stories“.
Inaaminika kuwa kwenye maboresho hayo mtu atakuwa na uwezo wa kuonyesha kupendezwa na chapisho husika mara nyingi tuu (zaidi ya mara moja). Pia, aliyechapisha hata pokea ujumbe wa kumwambia fulani na fulani wamependa kile alichokiweka kwenye “Stories” lakini itakuwepo sehemu ambayo mhusika ataweza kufahamu kile alichokiweka kimewapendeza wangapi.
Actually you can put a like multiple times 👇🏻 pic.twitter.com/uPEa2gmgnm
— Alessandro Paluzzi (@alex193a) August 23, 2021
Kwa sasa kipengele hiki bado hakijaanza kuonekana/kufanya kazi na pengine kikapatikana kwa wote au la! Hivyo, kitu cha kufanya ni kuendelea kutufuatilia na tutazidi kuwahabarisha yale yanayoendelea.
Chanzo: WaBetaInfo
No Comment! Be the first one.