Mtandao wa jamii maarufu duniani katika masuala ya picha umebadilisha vipengele katika mikataba na watumiaji wake vilivyokuwa vinaruhusu utumiaji wa picha za watumiaji kibiashara bila idhini yao.
Kampuni hiyo ya Instagram ilinunuliwa na Facebook na katika hatua za mwanzo inasemekani uongozi mpya unakuna ni jinsi gani watatengeneza faida kupitia huduma za Instagram.
Baada ya kutangaza mabadiliko ya mkataba na watumiaji ambayo yalikuwa yaanze kazi hapo mwezi wa kwanza mamilioni ya watumiaji duniani kote walianza kuishambulia Instagram kwa uamuzi huo na watafiti wengi walitabiri Instagram ingepoteza mamilioninya watumiaji hadi kufukia mwezi huo. Masaa machache baadae kampuni hiyo imeondoa mabadiliko hayo.
Mabadiliko hayo kama yasingebadilisha yangeruhusu kampuni hiyo kuuza picha mbalimbali zinazoweka na watumiaji mamilioni duniani kote katika mtandao huo. Watu wote ambao akaunti zao zime’setiwa’ “public” ndo wangeathirika na utaratibu huo, wakati wale ambao akaunti zao ni “private” wangekuwa salama.
Je Instagram ni Nini?
Instagram ni mtandao wa kijamii unaofanya kazi katika mfumo wa watumiaji ku’upload’ picha ikiwa na uwezo wa kuchagua ‘effects’ za kuweka kwenye hizo picha katika kuziboresha kimuonekano. Kisha marafiki, au watu wengine wanauwezo wa kuzipenda kwa kuzipa ‘Likes’ na pia wanauwezo wa kuacha maoni. Pia hawana uwezo wa kuzishusha/’download’ kuweka kwenye simu zao au tablets. App ya Instagram inapatikana kwa ajili ya smartphones mbalimbali zinazotumia mfumo wa iOs (apple), Android, na Windows OS.
No Comment! Be the first one.