Instagram wanazidi kujiweka katika hali nzuri kwa kutotegemea maendelea kupitia app ya Instagram tuu, timu hiyo imekuja na app nyingine ya kutungeneza video fupi za sekunde moja zenye ubunifu wa kuvutia.
App hiyo inafahamika kwa jina la Boomerang na inamsaidia mtumiaji kurekodi video fupi ya sekunde moja kisha app hiyo inaifanya iende taratibu na kuirudia rudia na hivyo kuweza kutengeneza kitu kama GIF, yaani ‘animated video’. Ingawa unarekodi video ya sekunde 1 app hiyo kupitia kuitengeneza video hiyo katika mfumo wa kujirudia inapatikana video ya sekunde 4.
Baada ya kutengeneza video hiyo unaweza kuipost kwenye akaunti yako ya Instagram, Facebook na kwingineko.
Video zinazotengenezwa kupitia app hiyo zinakuwa hazina sauti na pale zitakapochezwa zinakuwa zinaonesha tukio likienda mbele na kurudisha nyuma taratibu. Video fupi zimejipatia umaarufu sana hasa kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Instagram, na Vine. Kwa sasa sehemu ya video ndefu inaonekana kuwa ni YouTube tuu na kidogo, Facebook.
Hii ni app ya tatu kutoka timu ya Instagram, app zao zingine ni pamoja na Hyperlapse na Layout.
Kupakua app ya Boomerang kwa watumiaji wa Android -> Google Play | iOS -> App Store
Soma pia – Instagram Wakuletea App Mpya – Hyperlapse
One Comment